MAOMBI YA FUNGUA MALANGO NA MILANGO-7 Mara baada ya kukufndisha juu ya FUNGUO TANO za kufungua malango na milango, sasa nataka nikufundishe juu ya kipengele kingine ambacho ni ; SILAHA NANE ZA KUFUNGUA MILANGO NA MALANGO YALIYOFUNGWA MBELE YAKO; Maombi yetu ya Kufungua Milango na Malango yaliyofungwa inahitaji Uhodari na Uthabiti katika Imani, hivyo lazima silaha hizi zitumike ndipo Milango na Malango yaliyofungwa yatafunguliwa. Kufungua kilichofungwa si kazi rahisi. Maandiko matakatifu yanasema; “Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani; kwa maana kushindana kwetu si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa Roho, kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.” Waefeso 6:10-14 Maisha yetu ya Kristo yapo katika mgonga...