MATATIZO YA IMMA MJUZI KOMPYUTA NA NAMNA YA KUYAEPUKA INSI YA KUTATUA TATIZO HILI LA KUHARIBIKA KWA UBAO MAMA(MOTHERBOARD). 1. Utatuzi wa Shida(troubleshooting), (i) Angalia kama kuna “signal” zinazoonesha kama umeme unaingia kwenye Motherboard, hapa angalia kwenye “Power jeck” kama umeme unaingia kwenye motherboard. (ii) Pima “component” mbalimbali zinazounda mfumo mzima wa ubao mama, moja baada ya nyingine kwa kutumia kifaa kinachoitwa “Multimeter, ukigundua “component” ambayo ni mbovu waweza kuibadilisha. Kabla ya kuibadilisha hiyo “Component” yafaa ukaangalia vitu vifuatavyo; - Uthamani/ufanano wa “component” unazotaka kubadilisha. - Utendaji wa kazi wa “component” hiyo. (iii) Kuibadilisha “component” hiyo. Hapa utaamua kuibadilisha component hiyo kwa kuweka “component” nyingine ambayo ni nzima kama ilivyokuwa mwanzoni. (iv) Fanya usafi kwenye Ubao mama(Motherboard) pamoja na Kompyuta nzima kwa ujumla. (v) Washa Kompyuta yako. 2. Kubadilisha Ubao Mama (Ubao Mama...
Changamoto zinazoikabili lugha ya Kiswahili katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Kila jitihada zinazofanywa katika kufikia malengo fulani huwa hakukosi changamoto. Katika jitihada za kufanya Kiswahili kuwa lugha ya kiteknolojia kumetokea changamoto nyingi, moja wapo iliyo kuu kabisa ni kwamba lugha ya Kiswahili haimilikiwi na taifa lolote tajiri kwa hiyo katika harakatika za kuendeleza inakumbana na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa fedha na hata utayari wa viongozi wa kisiasa kukiendeleza Kiswahili ni mdogo sana, hata hivyo harakati hizi zinapingwa na mataifa ambayo lugha zao zimeendelea sana kiteknolojia kwa kuhofia kwamba zitafunikwa na matumizi ya Kiswahili. Wapo tayari kutoa misaada ili kuendeleza lugha zao kukididimiza Kiswahili kitu ambacho kinafanya harakati za kukiendeleza Kiswahili kuwa ngumu kwani nchi kinamozungumzwa Kiswahili hazina pesa za kupambana na mataifa makubwa yanayopigia upatu lugha zao. Kutokana na sababu hizo, kasi ya uundaji wa istilahi za kiteknolo...