Unapogundua simu yako ya Android smartphone imeingiliwa na virus ni vizuri kuhakikisha unaondoa haraka ili kupunguza hatari ya data zako kwenye simu kuharibiwa au kupotea kabisa.
Hapa nataka kukuelekeza jinsi ya kuondoa virus kwenye simu yako ya Android smartphone.
Kama unafikiri au umegundua kuwa simu yako imeingiliwa na virus, moja kati ya free antivirus programs kwa ajili ya simu za Android ni: AVG AntiVirus.
1. kitu cha kwanza kufanya ni kupakua (download) na ku-install AVG Antivirus kutoka Google Play au INGIA HAPA
2.Baada ya kuwa umekubali (accepted) permissions, umepakua (download) na ku-install hiyo application, ifungue. Activate application na click kwenyeProtection option.
3.Halafu, kwenye orodha ya options, click kwenye "Scan Now". Application itaanza ku-scan mafaili yote yaliyomo kwenye simu yako.
4.Antivirus hii itatafuta viruses na malware ambao wapo kwenye simu yako ya Android smartphone au tablet na baada ya kumaliza itawatoa virus wote.
5. Ili kuhakikisha simu yako inakuwa kwenye usalama siku zote unashauriwa kuendesha (run) antivirus mara moja kwa wiki. Na ni vizuri kutumia antivirus hii wakati simu yako ikiwa imeunganishwa kwenye power supply yaani ikiwa kwenye chaji au ikiwa na chaji fully.
Hii ndio njia ya haraka na yenye ufanisi kusafisha na kulinda simu yako ya android smartphone isidhurike na virus.
Nipende kushukuru kwa maelezo mazuri napenda kuyafanyia kazi coz cm yangu inanisumbua sana.....
JibuFuta