Changamoto zinazoikabili lugha ya Kiswahili katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Kila jitihada zinazofanywa katika kufikia malengo fulani huwa hakukosi changamoto. Katika jitihada za kufanya Kiswahili kuwa lugha ya kiteknolojia kumetokea changamoto nyingi, moja wapo iliyo kuu kabisa ni kwamba lugha ya Kiswahili haimilikiwi na taifa lolote tajiri kwa hiyo katika harakatika za kuendeleza inakumbana na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa fedha na hata utayari wa viongozi wa kisiasa kukiendeleza Kiswahili ni mdogo sana, hata hivyo harakati hizi zinapingwa na mataifa ambayo lugha zao zimeendelea sana kiteknolojia kwa kuhofia kwamba zitafunikwa na matumizi ya Kiswahili. Wapo tayari kutoa misaada ili kuendeleza lugha zao kukididimiza Kiswahili kitu ambacho kinafanya harakati za kukiendeleza Kiswahili kuwa ngumu kwani nchi kinamozungumzwa Kiswahili hazina pesa za kupambana na mataifa makubwa yanayopigia upatu lugha zao.
Kutokana na sababu hizo, kasi ya uundaji wa istilahi za kiteknolojia imekuwa ndogo sana, kwani kufanya hivyo pia kunahitaji pesa, na mara nyingi pesa zimekuwa zikitolewa na wahisani au makampuni yanayohusika kitu kinachotokea mara moja baada ya muda mrefu sana.
Pia, viongozi wa serikali hawajatilia mkazo suala hili, hawajaona umuhimu wa kukiendeleza Kiswahili kitenolojia. Nguvu zao nyingi wameziweka katika miradi mingine ya kimaendeleo huku wakisahau kabisa kuwa Kiswahili pia kinahitaji kwenda sambamba na maendeleo hayo. Kwa hiyo hii imekuwa ni changamoto katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili.
Kwa kuwa istilahi hizi zimekuwa zikifanywa na watu tofautitofauti, ni muhimu kuwapo na jopo maalumu la kusanifisha istilahi hizi kabla hazijasamabazwa. Kwa kufanya hivi hakutakuwa na matumizi tofauti ya istilahi katika dhana moja. Hali hii inajitokeza sana endapo uundaji wa istilahi utakuwa umefanywa katika makundi tofauti.
Utayari wa watumiaji; watumiaji wengi wa lugha ya Kiswahili wamekuwa wakilalamika kuhusu kutumia programu za komyuta kwa lugha za Kiswahili. Madai yao ni kwamba istilahi za Kiswahili ni ngumu sana na hivyo si rahisi kuzitumia, kwa mfano, wengi wamezoea kusema password na kwa hiyo ukiwaambi kwamba password kwa Kiswahili huitwa nywila au mouse inaitwa puku watabaki wakikushangaa na watona kama unawapa kazi kubwa sana. Kwa hiyo hii nayo inasabaisha matumizi ya Kiswahili katika vifaa vya kiteknolojia hususani kompyuta kuwa hafifu.
MAOMBI YA MWENYE THAMBI : Ombi la mwenye dhambi ni gani?" Ombi la mwenye dhambi ni Ombi ambalo mtu huomba kwa Mungu wakati anapotambua ya kwamba yeye ni mwenye dhambi au ametenda thambi na anahitaji kusamehewa na Mwokozi. Kusema Ombi hili la mwenye dhambi haikamilishi tayari kila kitu. Ombi la mwenye dhambi hufanya kazi tu sawasawa linapokuwa limesimamia kile mtu anacho fahamu, anacho elewa, na kukubali kuhusu dhambi zake na hitaji la Wokovu. Hatua ya kwanza ya Ombi la mwenye dhambi ni kufahamu ya kwamba sisi sote ni wenye dhambi. Warumi 3:10 , “Kama ilivyoandikwa,ya kwamba,Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Bibilia inaonyesha wazi ya kwamba sisi sote tumefanya dhambi. Sisi sote ni wenye dhambi na tunahitaji rehema na msamaha toka kwa Mungu (Tito 3:5-7). Kwa ajili ya dhambi zetu,tunastahili adhabu ya milele (Mathayo 25:46). Ombi hili la mwenye dhambi ni kwa kutafuta neema badala ya hukumu. Ni ombi la kuulizia rehema badala ya hasira kuu.rehema ni kuhesabiwa haki
Maoni
Chapisha Maoni