Mahakama Kuu yaikana kampuni iliyomtoa Mbowe Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe Dar es Salaam. Mahakama Kuu imekana kuitambua kampuni ya Fosters Auctioneers and General Traders iliyohusika kuondoa vitu vya kampuni za Freeman Mbowe kwenye jengo la Shirika la Taifa la Nyumba (NHC). Hayo yalibainishwa jana na kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema, Peter Kibatala wakati wa usikilizwaji wa maombi yaliyofunguliwa na mlalamikaji huyo kupitia kampuni ya Mbowe Hotels Ltd dhidi ya NHC na kampuni hiyo ya udalali. Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo jana, pamoja na mambo mengine Mbowe aliiomba Mahakama iliamuru NHC na kampuni hiyo wamrejeshe katika jengo hilo pamoja na vifaa na mali zake zinazoshikiliwa na kampuni hiyo. Wakili Kibatala aliieleza Mahakama kuwa mteja wake aliondolewa katika jengo hilo kinyume na sheria. Alidai dalali aliyetumiwa na NHC kuziondoa kampuni za Mbowe katika jengo hilo hajasajiliwa na Mahakama kwa kuwa walimwandiki