Ruka hadi kwenye maudhui makuu

WAZAZI MBARONI KWA KUOZESHA WANAFUNZI

Wazazi mbaroni kwa kuozesha wanafunzi

POLISI mkoani Rukwa inawashikilia wazazi watatu, akiwemo mume na mke, kwa kuozesha watoto wao wa kike wenye umri wa miaka 15 waliokuwa wakisoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Chipu katika Kata ya Kasense kwenye Manispaa ya Sumbawanga.

Aidha, mmoja wa watoto hao aliyeozeshwa kijijini humo anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano huku mwanamume wake anayedaiwa kuwa ni mtoto wa mwalimu mstaafu, aitwae Daud Kwitwa, akidaiwa kutoroka.

Msichana mwingine na mwanamume aliyeozeshwa walitoroka kijijini humo na kwenda katika kitongoji cha Malangali, Manispaa ya Sumbawanga mkoani humo ambapo wanadaiwa kufunga ndoa Agosti katika Kanisa Katoliki la Roho Mtakatifu, Jimbo la Sumbawanga, lililopo kwenye kitongoji cha Malangali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando, alithibitisha kukamatwa kwa wazazi hao na msichana mmoja, huku Polisi ikiendelea kumsaka msichana mwingine na mumewe. Wazazi waliokamatwa wametajwa kuwa ni Sabastian Sangu na mkewe Hilda Mizengo na mzazi mwingine wa kiume ni Misri Mwanakatwe.

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Dk Halfani Haule akizungumza na gazeti hili jana alisema walikamatwa Septemba 29, mwaka jana, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Shule ya Msingi Chipu akiwa ameongozana na Ofisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Sumbawanga, Frank Sichalwe.

“Nilipata taarifa ya kuwepo kwa watoro sugu shuleni hapo hivyo nilipofika niliingia darasa la sita nikaomba daftari la mahudhurio na kuanza kuwaita wanafunzi jina baada ya jina ndipo ilipobainika kuwa kati ya wanafunzi 142 wanaosoma darasa hilo, 52 ndio waliohudhuria huku 90 wakikosekana shuleni na kudaiwa kuwa watoro sugu,” Haule alisema.

Alisema alipodadisi zaidi wanafunzi wenyewe walianza kueleza kuwa wengi wa watoro wanafanya kazi za vibarua vya kuchunga ng’ombe na kwamba wasichana wawili wameolewa kijijini humo.

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAOMBI YA MWENYE DHAMBI

MAOMBI YA MWENYE THAMBI : Ombi la mwenye dhambi ni gani?" Ombi la mwenye dhambi ni Ombi ambalo mtu huomba kwa Mungu wakati anapotambua ya kwamba yeye ni mwenye dhambi au ametenda thambi na anahitaji kusamehewa na Mwokozi. Kusema Ombi hili la mwenye dhambi haikamilishi tayari kila kitu. Ombi la mwenye dhambi hufanya kazi tu sawasawa linapokuwa limesimamia kile mtu anacho fahamu, anacho elewa, na kukubali kuhusu dhambi zake na hitaji la Wokovu. Hatua ya kwanza ya Ombi la mwenye dhambi ni kufahamu ya kwamba sisi sote ni wenye dhambi. Warumi 3:10 , “Kama ilivyoandikwa,ya kwamba,Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Bibilia inaonyesha wazi ya kwamba sisi sote tumefanya dhambi. Sisi sote ni wenye dhambi na tunahitaji rehema na msamaha toka kwa Mungu (Tito 3:5-7). Kwa ajili ya dhambi zetu,tunastahili adhabu ya milele (Mathayo 25:46). Ombi hili la mwenye dhambi ni kwa kutafuta neema badala ya hukumu. Ni ombi la kuulizia rehema badala ya hasira kuu.rehema ni kuhesabiwa haki

CHANGAMOTO KATIKA LUGHA YA KISWAHILI KWENYE MAMBO YA KOMPYUTA (TEHAMA)

Changamoto zinazoikabili lugha ya Kiswahili katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Kila jitihada zinazofanywa katika kufikia malengo fulani huwa hakukosi changamoto. Katika jitihada za kufanya Kiswahili kuwa lugha ya kiteknolojia kumetokea changamoto nyingi, moja wapo iliyo kuu kabisa ni kwamba lugha ya Kiswahili haimilikiwi na taifa lolote tajiri kwa hiyo katika harakatika za kuendeleza inakumbana na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa fedha na hata utayari wa viongozi wa kisiasa kukiendeleza Kiswahili ni mdogo sana, hata hivyo harakati hizi zinapingwa na mataifa ambayo lugha zao zimeendelea sana kiteknolojia kwa kuhofia kwamba zitafunikwa na matumizi ya Kiswahili. Wapo tayari kutoa misaada ili kuendeleza lugha zao kukididimiza Kiswahili kitu ambacho kinafanya harakati za kukiendeleza Kiswahili kuwa ngumu kwani nchi kinamozungumzwa Kiswahili hazina pesa za kupambana na mataifa makubwa yanayopigia upatu lugha zao. Kutokana na sababu hizo, kasi ya uundaji wa istilahi za kiteknolo

KUROOT SIMU AINA ZOTE

NYUMBANI JINSI YA APPS MUHIMU PAKUA APP YETU Feb 15/2018   10 JINSI YA KUROOT SIMU YAKO HOW TO ROOT YOUR PHONE Nini maana ya kuroot?? Kuroot simu ni kitendo cha kuifanya simu iweze kufanya mambo ambayo hayawezi kufanyika katika mfumo wa kawaida wa android.    Nini faida ya kuroot simu yako? Kubadili mwandiko Kuweka custom ROM Kununua vitu bure katika apps Kufuta app zilizokuja na simu Kuondoa matangazo Kuongeza kasi ya simu Kupunguza matumizi ya battery Hasara za kuroot Kuondoa warranty Hutoweza kupata updates na ukipata hutoweza kuziinstall Uwezekano mkubwa wa kuharibu simu yako JINSI YA KUROOT Kuna njia nyingi za kuroot lakini njia hii nayoenda kukufundisha ndio njia nzuri zaidi! HATUA : Pakua KINGROOT  PAKUA HAPA Hakikisha umeunganishwa na mtandao wa internet Bonyeza "TRY ROOT" nasubiri mpaka itapofika 100% (Simu inaweza kuzima na kuwaka wakati wa hatua hii, ni kitu cha kawaida na hakina madhara yoyote) Baada ya kumalizika utapokea ujumbe"ROOT SUCCESSF