Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

WAFUASI WAMTAKA MAALIM AITISHE MKUTANO KUMTAMBUA LIPUMBA

Wafuasi wataka Maalim aitishe mkutano kumtambua Lipumba Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad  Baadhi  ya wafuasi wa aliyekuwa mwenyekiti wa CUF wamesema ili Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad aweze kuingia katika ofisi za makao ya CUF Buguruni ni lazima aitishe mkutano na wanahabari kumtambua Profesa Lipumba. Baadhi ya wafuasi hapo wamekusanyika eneo la ofisi hiyo wakiwa na nia ya kumpokea Profesa Lipumba na kumzuia Maalim Seif endapo atafika. Akizungumza kwa niaba ya wenzake Juma Yassin amesema Maalim Seif ataendelea kubaki Zanzibar iwapo  hatataka kumtambua Profesa Lipumba ambaye ni mwenyekiti halali Kikatiba. "Tumesikia leo huenda akaja lakini ofisi  na asijisumbue tupo tayari kwa lolote hadi amtambue Profesa Lipumba," amesema Yassin ambaye ni mwenyekiti wa Tawi la Kosovo Manzese.

WAZAZI MBARONI KWA KUOZESHA WANAFUNZI

Wazazi mbaroni kwa kuozesha wanafunzi POLISI mkoani Rukwa inawashikilia wazazi watatu, akiwemo mume na mke, kwa kuozesha watoto wao wa kike wenye umri wa miaka 15 waliokuwa wakisoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Chipu katika Kata ya Kasense kwenye Manispaa ya Sumbawanga. Aidha, mmoja wa watoto hao aliyeozeshwa kijijini humo anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano huku mwanamume wake anayedaiwa kuwa ni mtoto wa mwalimu mstaafu, aitwae Daud Kwitwa, akidaiwa kutoroka. Msichana mwingine na mwanamume aliyeozeshwa walitoroka kijijini humo na kwenda katika kitongoji cha Malangali, Manispaa ya Sumbawanga mkoani humo ambapo wanadaiwa kufunga ndoa Agosti katika Kanisa Katoliki la Roho Mtakatifu, Jimbo la Sumbawanga, lililopo kwenye kitongoji cha Malangali. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando, alithibitisha kukamatwa kwa wazazi hao na msichana mmoja, huku Polisi ikiendelea kumsaka msichana mwingine na mumewe. Wazazi waliokamatwa wametajwa kuwa ni Sabastian Sangu na mkewe Hild...

NDALICHAKO APIGWA NA WAALIMU

Ndalichako apingwa na walimu Maswa. Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani hapa, Mkoa wa Simiyu, kimemjia juu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako kuwa anaupotosha umma juu ya madai yao. Kimesema walimu wanadai madeni mengi, hivyo kauli ya Ndalichako kwamba hawana wanachodai inalenga kuleta uchonganishi kati yao na Serikali. Mwenyekiti wa CWT wilayani hapa, Onesmo Makota amesema wao wanaidai Serikali zaidi ya Sh500 milioni kutokana na malimbikizo na mapunjo ya mishahara.

Magazeti ya leo september 28

Magazeti ya Leo September 28.9.2016 Magazeti ya Leo September 28.9.2016...

Serikali kuzindua leo ndege mpya

September 27, 2016 VIDEO: Ndege mpya ya pili ya Air Tanzania ilivyowasili jijini Dar es salaam Newsroom TZA Baada ya ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuwasili nchini September 20 2016, Leo September 27 2016  ndege yapili ya Bombadier Q400 imewasili Dar es salaam ikitokea Canada baada ya ile ya kwanza ambazo zimenunuliwa na serikali. Naambiwa kuwa uzinduzi rasmi wa ndege hizo utafanyika kesho jumatano September 28 2016 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere Dar es salaam. ULIKOSA HII NDEGE MPYA YA KWANZA ILIVYOWASILI JIJINI DAR ES SALAAM? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

LUKUVI AFUTA HATI TATU MAKABURI KINYERENZI

Serikali yafuta hati 3 eneo la makaburi kinyerezi Wakazi wa Kinyerezi Sokoni, Dar es Salaam wameipongeza Serikali ya awamu ya Tano kwa kufuta hati tatu zilizokuwazimetolewa katika eneo la makaburi liliouzwa kinyume cha sheria. Pongezi hizo zimetolewa leo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi baada ya kumwagiza kamishna wa ardhi Kanda ya Dar es Salaam kufuta hati hizo mara moja na kulirejesha eneo la makaburi kwa wananchi. Akiongea kwa niaba ya wakazi wa Kinyerezi, Mwanasheria, Mwinjuma Mzee amesema kuwa Wanakinyerezi wanamshukuru sana Mhe. Waziri kwa kurejesha eneo la makaburi kwa wakazi hao. “Mhe. Waziri na msafara wake wote tunawashukuru kwa kumaliza mgogogoro huu ambao umedumu kwa muda mrefu na tumemwomba Waziri ashughulikie na maeneo mengine yanayohusu huduma za jamii kama zahanati na shule,” alisema Mzee. Naye mkazi wa Kinyerezi, Bi. Maimuna Forogo ameelezea furaha yake kwa kumshukuru sana Mhe waziri kwa hatua aliyoichukua ya kuba...

MATUMAINI WIZARA YA DAWA

Wizara yasema dawa zinapatikana kwa asilimia 53 Dar es Salaam. Serikali kupitia Wizara ya Afya imewaondoa wasiwasi watanzania kuhusu uhaba  wa dawa nchini na kueleza kuwa dawa zinapatikana kwa asilimia 53. Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk Mpoki Ulisubisya amesema hali ya upatikanaji wa dawa itaimarika zaidi mwanzoni mwa Oktoba. Amesema kati ya dawa muhimu 135 zinazohitajika,ghalani zipo aina 71 na nyingine zipo kwenye vituo vya kutolea huduma.