Kuna maswali mengi sana unopo mtaja yesu ila naomba ufuatane pamoja nami hatua moja hadi nyingile ili tumjue yesu ni nani karibia miaka 2.000 iliyopita Yesu aliwauliza wanafunzi wake maswali maswali mawili ambayo mpaka sasa yamo ndani ya Mioyo na fikra za wanaadamu
1."watu hunena kuwa mwana wa adamu kuwa ni nani?"
2.na ninyi mwanena mm kuwa ni nani?"matayo .16:13-16 watu wengi,dini nyingi na hata wasomi wengi(ma-filosofa)wamejaribu kutoa majibu kadhaa katika kujibu swali la kwanza .baadha ya watu wengine walijibu kuwa yu nabii,na kwa wengine yesu alikuwa mwalimu mkuu na bado kwa wengine alikuwa mtu mwema na mwadilifu ambaye mfano wa maisha yake unastahili kuigwa.
Lakini jawabu la swali la pili ni muhimu sana.maana katika jawabu la kila mtu binafsi,ndipo pale penye hatima ya milele (Yohana3:36)lakini haina maana na mawazo ya maisha ya wakati huu(Yohana 10:10;wakolosai3:3-4;wagalatia2:20) hivyo basi kiini na fikra za ki-thiolojia yaliyoenea tangu zama na zama yamekuwa,na mpaka sasa ndivyo yalivyo,kwamba;“nani yesu kristo?" Na kwahiyo biblia inasema kuwa yesu kristo yu nani -Mungu katika hali ya ki-binaadamu-watu wote kila mahali inabidi wajishuhulishe mno na dini, lakini wakae waishi katika uhusiano mwema na mungu kupitia yesu kristo (yohana 14:6 ) kwahiyo basi hakuna elimu nyingine ya kujifunza isipokuwa elimu ya kristo. Kwasababu yesu alichukua hali ya u-binaadamu(wafilipi2:5-11)ili awe na uwezo wa kuwaeleza wanaadamu,siyo tu mungu ni nani na jinsi alivyo(yohana1:18)bali pia kuonyesha kuwa mwanadamu ni nani na jinsi ambavyo mungu anahitaji huyo mwanaadamu awe wa namna gani(1petro2:21;1wakor15:45-49) kwahiyo kujifunza elimu ya kidini kuhusu kristo hufunua mengi kuhusu mungu na mwanaadamu najinsi mwanaadamu anavyoweza kuwasiliana na mungu na kadhalika wanaadamu wengine.basi ilivyo,kujifunza kwetu elimu ya dini kutalenga kwa namna ya kipekee yale biblia inavyo fundisha kuhusu yesu kristo
VIFUNGU MUHIMU KUHUSU KRISTO
Huku kukiwa na vifungu muhimu vingi kuhusu yesu kristo,vifuatavyo ni vifungu maalumu muhimu vinavopasa kusomwa kwa uangalifu sana.
Yohana1:1-18
Warumi5:12-20
waefeso1:3-10
Wafilipi2:5-11
Wakolosai1:15-22
Wakolosai2:9-15
Waebrania1:1-9
Vifungu hivyi ni vya muhimu mno katika mafundisho kuhusu Yesu na mambo yale aliyojia kuyatenda ulimwenguni.
Hali ya
Maoni
Chapisha Maoni