MWANAMUZIKI MTANZANIA MWENYE ASILI YA ITALIA KUTUMBUIZA HOTELI YA MEDITERRANEO JUMAMOSI HII JIJINI DAR
Dotto Mwaibale
Mwanamuziki wa miondoko ya Jazz kutoka nchini Italia Mwenye asili ya Tanzania Chantal Saroldi anataraji kutumbuiza katika Hafla maalumu ya kusherehekea Siku ya Taifa la Italia ambapo raia wa Italia waishio nchini watajumuika pamoja kwenye viunga vya ubalozi wa Italia ili kusherehekea Siku hiyo.
Mwanamuziki Chantal Saroldi mwenye asili ya Italia na Tanzania alizaliwa nchini Tanzania katika mkoa wa Kilimanjaro akitokea kabila la Wachaga.
Chanty yupo nchini kwa ajili ya ziara maalumu ya Muziki ambapo kesho anatarajia kutumbuiza katika hoteli ya Mediterraneo ya jijini Dar esalaam na Juni 2 anataraji kutumbuiza katika hafla maalumu inayoandaliwa na ubalozi wa Italia nchini ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Taifa hilo.
Balozi wa Italia nchini Tanzania, Luigi Scotto, alisema kuwa katika kuzingatia kuwa mwanadada Chantal ni mwanamuziki mahiri waratibu wa sherehe hizo wamemchaguliwa kuja kutumbuiza katika hafla hiyo kwa kuwa ni nembo muhimu inayoziunganisha nchi mbili hizi za Tanzania na Italia.
Katika hatua nyingine mwanadada huyo alisema kuwa anajilaumu kwa kutojifunza lugha ya mama yake ambayo ni kiswahili, huku akibainisha kuwa mikakati ni kujifunza lugha ya Kiswahili.
Mwanamuziki huyo amewahi kushinda tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya dhahabu katika kipengele cha uhariri na uandishi wa nyimbo ikitolewa na Disc Festival.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
Maoni
Chapisha Maoni