Uchaguzi katika majimbo mbalimbali ya Uchaguzi mkoani Morogoro, wameendelea kuwa na kigugumizi juu ya kutangaza matokeo ya uchaguzi katika maeneo yao huku wakibainisha kuwa changamoto za kijiografia katika maeneo mengi kukwamisha hali hiyo kufanyika kwa wakati. Hata hivyo, katika majimbo mbalimbali ya uchaguzi, Chama Cha Mapinduzi kimeonekana kujizolea viti vingi vya udiwani ingawa maeneo mengine wagombea wake wameshindwa kutetea nafasi zao na viti hivyo kunyakuliwa na wagombea wa vyama vya upinzani vikiwamo vile vinavyoungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na ACT- Wazalendo. Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mvomero, Wallace Karia, alisema jimbo hilo lina kata 30, lakini moja ya Mvomero haikufanya uchaguzi baada ya mgombea wake mmoja wa udiwani kufariki dunia wakati wa mchakato wa kampeni. Alisema kati ya kata 30, kata 22 zimenyakuliwa na CCM huku kata mbili za ...