Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Uchaguzi

Habari za kosiasa karibu
Tanzania

UCHAGUZI 2015: Matokeo ya uchaguzi ngazi ya Rais
yataanza kutangazwa kwa awamu ya kwanza saa tatu
asubuhi, saa sita mchana, saa tisa na saa 12 jioni.
UCHAGUZI 2015: Wagombea urais wa vyama vya CCM na
Chadema wanachuana vikali kwa mujibu wa matokeo ya
awali yanayotangazwa kwenye vituo mbalimbali nchini
MATOKEO URAIS Z’BAR: Kwa mujibu wa NEC, Dk Shein
(CCM) ameongoza katika jimbo la Kiembesamaki kwa kura
4,413 dhidi ya 2,986 za Maalim Seif (CUF)
MATOKEO URAIS Z’BAR: Hadi sasa ZEC imetangaza
matokeo ya urais katika majimbo ya Fuoni na Kiembesamaki
na Shein (CCM) anaongoza dhidi ya Maalim Seif (CUF)
MATOKEO URAIS Z’BAR: ZEC yatangaza kuwa Jimbo la
Fuoni; Dk Shein (CCM) amepata kura 889 wakati Maalim Seif
(CUF) akiwa na kura 429. Waliojiandikisha kupiga kura jimbo
katika jimbo hilo ni 1,822, waliopiga kura ni 1,397.
CHADEMA: Imethibitika kuwa tulichokibashiri kimetokea.
Hivyo tuna haki ya kulinda kura zetu.
CHADEMA: Dosari za uchaguzi Katavi, Kimara na Pemba
zinadhihirisha kuwa uchaguzi huu si huru na haki
ARUMERU: Msimamizi mkuu wa kituo cha Arumeru
Magharibi, Fidelis Lumato amesema kuwa wanashukuru
wamemaliza uchaguzi salama bila vurugu hivyo wanaomba
wananchi waendelee hivyo hadi kesho asubuhi
atakapotangaza matokeo ya jumla.
MUSOMA: Polisi watumia mabomu ya machozi kutawanya
wananchi wanaovunja kituo cha kuhesabia kura cha Kigera,
Musoma Mjini wakipinga matokeo yanayotangazwa
IFAKARA: Polisi wapiga mabomu ya machozi baada ya vijana
kufanya fujo kwa kurusha mawe juu ya majengo ya shule ya
msingi Mhola.
MVOMERO: Wasimamizi katika kituo cha shule ya msingi
Wami Sokoine wakitumia simu za tochi na karabai kwa ajili
ya uhesabuji kura. KJusoma zaidi bofya
TUNDUMA: Mawakala Jimbo la Tunduma wanyang’anywa
simu na wasimamizi baada ya kubainika wakirusha matokeo
kwa wenzao nje. Na kutokana na hali hiyo wananchi
wameanza kukusanyika kwa wingi jirani na vituo vya
kuhesabia kura huku wakiimba nyimbo za vyama vyao.
ARUMERU: Kata ya Maivo kituo cha sokoni Jimbo la
Arumeru watu bado wako kwenye foleni wanapiga kura na
hii ni baada ya majina zaidi ya 200 kukosekana kwenye
orodha ya wapiga kura.
Msimamizi wa kituo cha skuli ya Mtambile, jimbo la
Mtambile, mkoa wa Kusini Pemba, Hafidhi Said Ali
akionyesha tochi itakayotumika usiku wa kuhesabu kura
kituoni hapo.
AWE: Zoezi la kuhesabu kura bado linaendelea katika vituo
mbalimbali vya Jimbo la Kawe.Katika kituo cha Bunju A,
zoezi la kuhesabu kura za urais lilirudiwa baada ya wakala
wa CCM kutoridhishwa na matokeo ya mgombea wake.
Zoezi la kuhesabu kura linaendelea kituo cha Uwanja wa
soko Mageuzi Jimbo la Shinyanga mjini.
KIGOMA: Kigoma Kusini hali ni shwari, watu wapo
wajumbani wanasubiri matokeo, hata baa hazina watu mji
umetulia.
KARATU: Karatu waanza kuhesabu kura katika madarasa ya
shule hakuna umeme wanatumia tochi.
SERENGETI: Zoezi la kuhesabu kura Jimbo la Serengeti
linaendelea, shamrashamra baadhi ya mitaa ikianza licha ya
mvua kubwa inayonyesha.
LINDI: Mkazi wa kijiji cha Kiangara wilaaya ya Liwale mkoani
Lindi Abreheman Mkopora anashikiliwa na polisi kwa
tuhuma ya kutaka kujiandikisha mara mbili.
NYAMAGANA: Kituo cha shule ya msingi Mbugani Jimbo la
Nyamagana kuna vijana wanalinda kura
Baadhi ya wakazi wa Kinyerezi wakimhoji askari Magereza
katika kituo cha shule ya msingi Mount Pleasant baada ya
kuona gari ndogo mabayo imeelezwa kuwa ni ya mlinzi
inaingizwa ndani ya kituo hicho wakati kura zinahesabiwa
ndani. Waliingia ndani na kupekua gari hilo.
TEMBONI: Kituo cha shule ya msingi Temboni hadi sasa
watu zaidi ya 400 hawajapiga kura majina yao hayaonekani
kwenye daftari, zoezi limesitishwa watu wameambiwa
watawanyike wamegoma.
TUNDUMA: Wananchi Jimbo la Tunduma wamenza
kusimama kando kando mwa vituo vya kuhesabia kura na
kila gari linalopita jirani na vituo wanazuia na kulirudisha
lilikotoka. Wanasema hawamuamini mtu yeyote anayekatiza
eneo hilo.
Wananchi wa kata ya Uwanjani wakiwa kwenye uwanja wa
Moira wa shule ya msingi Tunduma wakisubiria matokeo,
polisi wamewaambia wakusanyike hapo baada ya kuona
wanasogea na kujikusanya jirani na vituo vya kupigia kura.
MOSHI: Gari la mmoja wa makampeni meneja wa mgombea
ubunge Jimbo la Moshi vijijini (CCM), Dk Cyrill Chami,
limeshambuliwa na kuharibiwa vibaya na wananchi
wakilishuku kuwa na kura bandia.
MWANZA: Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Tito
Mahinya anasema kuanzia saa 6:00 usiku wataanza kutoa
matokeo ya jumla ya udiwani Jimbo la Nyamagana.
LULINDI: Jimbo la Lulindi wananchi wameshindwa kupiga
kura ya nafasi ya ubunge hivyo uchaguzi wa nafasi hiyo
umeahirishwa, ni baada ya kukosewa majina ya mgombea
wa CUF katika wa CUF katika karatasi ya kupigia kura.
MAHANAIMU.COM

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAOMBI YA MWENYE DHAMBI

MAOMBI YA MWENYE THAMBI : Ombi la mwenye dhambi ni gani?" Ombi la mwenye dhambi ni Ombi ambalo mtu huomba kwa Mungu wakati anapotambua ya kwamba yeye ni mwenye dhambi au ametenda thambi na anahitaji kusamehewa na Mwokozi. Kusema Ombi hili la mwenye dhambi haikamilishi tayari kila kitu. Ombi la mwenye dhambi hufanya kazi tu sawasawa linapokuwa limesimamia kile mtu anacho fahamu, anacho elewa, na kukubali kuhusu dhambi zake na hitaji la Wokovu. Hatua ya kwanza ya Ombi la mwenye dhambi ni kufahamu ya kwamba sisi sote ni wenye dhambi. Warumi 3:10 , “Kama ilivyoandikwa,ya kwamba,Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Bibilia inaonyesha wazi ya kwamba sisi sote tumefanya dhambi. Sisi sote ni wenye dhambi na tunahitaji rehema na msamaha toka kwa Mungu (Tito 3:5-7). Kwa ajili ya dhambi zetu,tunastahili adhabu ya milele (Mathayo 25:46). Ombi hili la mwenye dhambi ni kwa kutafuta neema badala ya hukumu. Ni ombi la kuulizia rehema badala ya hasira kuu.rehema ni kuhesabiwa haki

CHANGAMOTO KATIKA LUGHA YA KISWAHILI KWENYE MAMBO YA KOMPYUTA (TEHAMA)

Changamoto zinazoikabili lugha ya Kiswahili katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Kila jitihada zinazofanywa katika kufikia malengo fulani huwa hakukosi changamoto. Katika jitihada za kufanya Kiswahili kuwa lugha ya kiteknolojia kumetokea changamoto nyingi, moja wapo iliyo kuu kabisa ni kwamba lugha ya Kiswahili haimilikiwi na taifa lolote tajiri kwa hiyo katika harakatika za kuendeleza inakumbana na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa fedha na hata utayari wa viongozi wa kisiasa kukiendeleza Kiswahili ni mdogo sana, hata hivyo harakati hizi zinapingwa na mataifa ambayo lugha zao zimeendelea sana kiteknolojia kwa kuhofia kwamba zitafunikwa na matumizi ya Kiswahili. Wapo tayari kutoa misaada ili kuendeleza lugha zao kukididimiza Kiswahili kitu ambacho kinafanya harakati za kukiendeleza Kiswahili kuwa ngumu kwani nchi kinamozungumzwa Kiswahili hazina pesa za kupambana na mataifa makubwa yanayopigia upatu lugha zao. Kutokana na sababu hizo, kasi ya uundaji wa istilahi za kiteknolo

KUROOT SIMU AINA ZOTE

NYUMBANI JINSI YA APPS MUHIMU PAKUA APP YETU Feb 15/2018   10 JINSI YA KUROOT SIMU YAKO HOW TO ROOT YOUR PHONE Nini maana ya kuroot?? Kuroot simu ni kitendo cha kuifanya simu iweze kufanya mambo ambayo hayawezi kufanyika katika mfumo wa kawaida wa android.    Nini faida ya kuroot simu yako? Kubadili mwandiko Kuweka custom ROM Kununua vitu bure katika apps Kufuta app zilizokuja na simu Kuondoa matangazo Kuongeza kasi ya simu Kupunguza matumizi ya battery Hasara za kuroot Kuondoa warranty Hutoweza kupata updates na ukipata hutoweza kuziinstall Uwezekano mkubwa wa kuharibu simu yako JINSI YA KUROOT Kuna njia nyingi za kuroot lakini njia hii nayoenda kukufundisha ndio njia nzuri zaidi! HATUA : Pakua KINGROOT  PAKUA HAPA Hakikisha umeunganishwa na mtandao wa internet Bonyeza "TRY ROOT" nasubiri mpaka itapofika 100% (Simu inaweza kuzima na kuwaka wakati wa hatua hii, ni kitu cha kawaida na hakina madhara yoyote) Baada ya kumalizika utapokea ujumbe"ROOT SUCCESSF