Ruka hadi kwenye maudhui makuu

UCHAGUZI MKUU 2015

Uchaguzi katika majimbo mbalimbali ya
Uchaguzi mkoani Morogoro, wameendelea kuwa na
kigugumizi juu ya kutangaza matokeo ya uchaguzi katika
maeneo yao huku wakibainisha kuwa changamoto za
kijiografia katika maeneo mengi kukwamisha hali hiyo
kufanyika kwa wakati.
Hata hivyo, katika majimbo mbalimbali ya uchaguzi, Chama
Cha Mapinduzi kimeonekana kujizolea viti vingi vya udiwani
ingawa maeneo mengine wagombea wake wameshindwa
kutetea nafasi zao na viti hivyo kunyakuliwa na wagombea
wa vyama vya upinzani vikiwamo vile vinavyoungwa mkono
na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na ACT-
Wazalendo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu
ya Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Msimamizi wa
Uchaguzi wa Jimbo la Mvomero, Wallace Karia, alisema
jimbo hilo lina kata 30, lakini moja ya Mvomero haikufanya
uchaguzi baada ya mgombea wake mmoja wa udiwani
kufariki dunia wakati wa mchakato wa kampeni.
Alisema kati ya kata 30, kata 22 zimenyakuliwa na CCM huku
kata mbili za Diongoya na Bunduki, wagombea wake walipita
bila kupingwa na saba zikichukuliwa na vyama vya upinzani.
Karia alisema kata zilizonyakuliwa na Chadema ni Chenzema,
Nyandira, Mtibwa na Hembeti zilizochukuliwa na chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema na Kikeo na Liwale
zikienda kwa ACT Maendeleo na kata ya Mangae ikichukuliwa
na CUF. Kwa matokeo ya ubunge ambayo katika jimbo hilo,
vyama sita ya CCM, Chadema, DP,ACTna UPDP
vilisimamisha wagombea.
Hata hivyo, alisema bado wanaendelea kujumlisha kwa njia
ya kilektroniki.
Lakini mchuano mkali ulikuwa ni kwa wagombea wa CCM na
Chadema.
Akizungumza kwa njia ya simu, Msimamizi wa Uchaguzi
Jimbo la Ulanga, zamani Ulanga Mashariki, Isabela
Chilumba, alisema wamefanya uchaguzi wa nafasi ya
madiwani na Raisi pekee, huku nafasi ya ubunge ikiachwa
hadi pale Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakapotangaza upya,
baada ya kutokea kifo cha aliyekuwa mgombea ubunge kwa
tiketi ya CCM, Celina Kombani.
Alisema jimbo hilo lina jumla ya kata 21, na sita zilichukuliwa
na Chadema, huku zilizobaki zikichukuliwa na CCM.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Malinyi zamani likiitwa
Ulanga Magharibi, Said Msomoka, alisema Dk. Haji Mponda,
aliyekuwa akitetea kiti chake kutoka CCM, alikuwa akiongoza
kwa kura nyingi ikilinganishwa na wapinzani wake.
Aidha, alisema kati ya kata 10 zilizopo kwenye jimbo hilo
jipya la uchaguzi, kata nne zilichukuliwa na Chadema
ikiwamo Kilosa kwa Mpepo, Bilo, Ngoheranga na Itete
Minazini, huku sita zilizosalia zikichukuliwa na CCM.
Msomoka alisema changamoto ya jiografia ya maeneo pia
iliwachelewesha kufanikisha majumuisho kwa haraka, hasa
kwa kata za Itete, Sofi na Kilosa kwa Mpepo kuchelewa
kufikisha matokeo.
Kwa upande wa Jimbo la Kilosa Kati lenye jumla ya kata 25,
Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo, Iddi Mshihiri, alisema
kata tatu zilichukuliwa na Chadema na 22 CCM, huku Jimbo
la Mikumi, kati ya kata 15 zilizopo, nne zilichukuliwa na
Chadema na nane CCM na kata tatu za Vidunda, Ulaya na
Kilangala, walichelewa kufikisha matokeo kutokana na
jiografia ya maeneo hayo.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kilombero na Mlimba
Azimina Mbilinyi, naye alikiri jiografia ya wilaya hiyo
kuchelewesha zoezi zima la kupata matokeo na majumuisho
ya kura na kwamba kwa vile njia ya uwekaji matokeo ni ya
njia ya kielektroniki, ilihitaji umakini wa hali ya juu ndipo
atangaze matokeo, jambo ambalo pia lilibainishwa na
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Gairo, Mbwana Magota,
aliyedai kata za Nongwe, Magoyeko na Chagongwe
zilisababisha zoezi hilo kuchelewa.
Aidha, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Morogoro Kusini
yenye kata 17 na Morogoro Kusini Mashariki yenye kata 14,
Yona Maki, alisema pia tatizo hilo la jiografia ya maeneo na
mvua iliyonyesha jana maeneo hayo, zilisababisha matokeo
kuchelewa kupatikana kwa wakati hususan jiografia katika
kata za Mkuyuni, Tegetero, Singisa na Bwakila Juu.
Manispaa ya Morogoro hali ilikuwa tofauti zaidi, ambapo
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Morogoro Mjini,Theresia
Mahongo, alipohojiwa sababu za kuchelewesha kutangaza
matokeo ilihali wapo mjini, alidai wana kata 29 ambazo ni
nyingi na baadhi ya maeneo zilizuka vurugu zilizosababisha
baadhi ya maeneo wasimamizi wa vituo na mawakala
kuahirisha zoezi la kuendelea kuhesabu hadi asubuhi na
kwamba kikwazo cha usafiri na jiografia ya maeneo kwa
manispaa hakikuwapo kabisa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAOMBI YA MWENYE DHAMBI

MAOMBI YA MWENYE THAMBI : Ombi la mwenye dhambi ni gani?" Ombi la mwenye dhambi ni Ombi ambalo mtu huomba kwa Mungu wakati anapotambua ya kwamba yeye ni mwenye dhambi au ametenda thambi na anahitaji kusamehewa na Mwokozi. Kusema Ombi hili la mwenye dhambi haikamilishi tayari kila kitu. Ombi la mwenye dhambi hufanya kazi tu sawasawa linapokuwa limesimamia kile mtu anacho fahamu, anacho elewa, na kukubali kuhusu dhambi zake na hitaji la Wokovu. Hatua ya kwanza ya Ombi la mwenye dhambi ni kufahamu ya kwamba sisi sote ni wenye dhambi. Warumi 3:10 , “Kama ilivyoandikwa,ya kwamba,Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Bibilia inaonyesha wazi ya kwamba sisi sote tumefanya dhambi. Sisi sote ni wenye dhambi na tunahitaji rehema na msamaha toka kwa Mungu (Tito 3:5-7). Kwa ajili ya dhambi zetu,tunastahili adhabu ya milele (Mathayo 25:46). Ombi hili la mwenye dhambi ni kwa kutafuta neema badala ya hukumu. Ni ombi la kuulizia rehema badala ya hasira kuu.rehema ni kuhesabiwa ...

KUROOT SIMU AINA ZOTE

NYUMBANI JINSI YA APPS MUHIMU PAKUA APP YETU Feb 15/2018   10 JINSI YA KUROOT SIMU YAKO HOW TO ROOT YOUR PHONE Nini maana ya kuroot?? Kuroot simu ni kitendo cha kuifanya simu iweze kufanya mambo ambayo hayawezi kufanyika katika mfumo wa kawaida wa android.    Nini faida ya kuroot simu yako? Kubadili mwandiko Kuweka custom ROM Kununua vitu bure katika apps Kufuta app zilizokuja na simu Kuondoa matangazo Kuongeza kasi ya simu Kupunguza matumizi ya battery Hasara za kuroot Kuondoa warranty Hutoweza kupata updates na ukipata hutoweza kuziinstall Uwezekano mkubwa wa kuharibu simu yako JINSI YA KUROOT Kuna njia nyingi za kuroot lakini njia hii nayoenda kukufundisha ndio njia nzuri zaidi! HATUA : Pakua KINGROOT  PAKUA HAPA Hakikisha umeunganishwa na mtandao wa internet Bonyeza "TRY ROOT" nasubiri mpaka itapofika 100% (Simu inaweza kuzima na kuwaka wakati wa hatua hii, ni kitu cha kawaida na hakina madhara yoyote) Baada ya kumalizika utapokea ujumbe"ROOT...

CHANGAMOTO KATIKA LUGHA YA KISWAHILI KWENYE MAMBO YA KOMPYUTA (TEHAMA)

Changamoto zinazoikabili lugha ya Kiswahili katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Kila jitihada zinazofanywa katika kufikia malengo fulani huwa hakukosi changamoto. Katika jitihada za kufanya Kiswahili kuwa lugha ya kiteknolojia kumetokea changamoto nyingi, moja wapo iliyo kuu kabisa ni kwamba lugha ya Kiswahili haimilikiwi na taifa lolote tajiri kwa hiyo katika harakatika za kuendeleza inakumbana na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa fedha na hata utayari wa viongozi wa kisiasa kukiendeleza Kiswahili ni mdogo sana, hata hivyo harakati hizi zinapingwa na mataifa ambayo lugha zao zimeendelea sana kiteknolojia kwa kuhofia kwamba zitafunikwa na matumizi ya Kiswahili. Wapo tayari kutoa misaada ili kuendeleza lugha zao kukididimiza Kiswahili kitu ambacho kinafanya harakati za kukiendeleza Kiswahili kuwa ngumu kwani nchi kinamozungumzwa Kiswahili hazina pesa za kupambana na mataifa makubwa yanayopigia upatu lugha zao. Kutokana na sababu hizo, kasi ya uundaji wa istilahi za kiteknolo...