Wednesday, November 4, 2015
Tupe Maoni Yako( Matusi
Hapana )
Mpekuzi blog
Serikali Yakanusha Taarifa za Kifo
cha Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa
Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Assah
Mwambene amekanusha taarifa zinazosambaa
katika mitandao ya kijamii kuhusu Rais Mstaafu,
Benjamin Mkapa kuwa amefariki Dunia.
Akizungunza na waandishi wa habari katika ukumbi
wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mwambene
amesema Rais Mkapa yupo salama na mzima wa
afya na hakuna maradhi yoyote yanayomsumbua.
Mwambene amewaasa watumiaji wa mitandao
mbalimbali hasa Blogs kuacha kuitumia mitandao
hiyo kwa kupotosha umma na kuandika nambo
yasiyo na ukweli ili kuepusha mifumuko ya habari
za upotishaji.
“Si jambo jema na wanaofanya hivyo waache mara
moja kabla ya hatua stahiki hazijachukuliwa,”
amesema Mwambene.
Amesema kuwa jambo la kumzushia mtu kifo si
jambo zuri ambalo amelizungumza kama ‘uchuro’
kwa mtu husika na kumtabiria mabaya.
“Mkapa yupo hai na kesho pia atakuwepo katika
sherehe za kumuapisha Rais mteule wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, John Magufuli,” amesema
Mwmbene na kuongeza.
Serikali italishughulikia hili na tayari imeshaanza
kukamata baadhi ya watu mbalimbali ambao
wanatoa taarifa za uongo zinazopelekea umma
kupotoka.
Amesema kuwa vyombo vya habari vifanye kazi
kwa uweredi ili kazi ya uandishi wao iwe ya usawa
na kufuata misingi ya uandishi, jambo ambalo
wengi hukiuka kutokana kutofuata weredi wa kazi
zao.
MAOMBI YA MWENYE THAMBI : Ombi la mwenye dhambi ni gani?" Ombi la mwenye dhambi ni Ombi ambalo mtu huomba kwa Mungu wakati anapotambua ya kwamba yeye ni mwenye dhambi au ametenda thambi na anahitaji kusamehewa na Mwokozi. Kusema Ombi hili la mwenye dhambi haikamilishi tayari kila kitu. Ombi la mwenye dhambi hufanya kazi tu sawasawa linapokuwa limesimamia kile mtu anacho fahamu, anacho elewa, na kukubali kuhusu dhambi zake na hitaji la Wokovu. Hatua ya kwanza ya Ombi la mwenye dhambi ni kufahamu ya kwamba sisi sote ni wenye dhambi. Warumi 3:10 , “Kama ilivyoandikwa,ya kwamba,Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Bibilia inaonyesha wazi ya kwamba sisi sote tumefanya dhambi. Sisi sote ni wenye dhambi na tunahitaji rehema na msamaha toka kwa Mungu (Tito 3:5-7). Kwa ajili ya dhambi zetu,tunastahili adhabu ya milele (Mathayo 25:46). Ombi hili la mwenye dhambi ni kwa kutafuta neema badala ya hukumu. Ni ombi la kuulizia rehema badala ya hasira kuu.rehema ni kuhesabiwa haki
Maoni
Chapisha Maoni