November 14, 2015 Mambo yameanza Dodoma, ratiba ya Bunge ni hii + pichaz Wabunge waliofika.. Newsroom TZA Kama umetembelea mitandao ya kijamii utakuwa umeona pilikapilika za kinachoendelea Dodoma sasahivi, baada ya Uchaguzi Mkuu kuisha wale wote waliopita kwenye nafasi ya Ubunge wanasubiri shughuli ya kuapishwa halafu Vikao vya Bunge vinaanza. Nimeipata Ratiba ya kitakachoendelea Dodoma kwa jumla ya siku saba mfululizo, yani kuanzia jana November 13 mpaka November 20 2015… Ratiba yenyewe hii hapa. Mbunge Mteule wa Jimbo Mwanga K’njaro, Prof. Jumanne Maghembe akiwasilisha nyaraka zake wakati wa kusajiliwa Bungeni Dodoma. Mbunge Mteule wa Sengerema, William Ngeleja nae kwenye foleni ya usajili katika Viwanja vya Bunge Dodoma
Changamoto zinazoikabili lugha ya Kiswahili katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Kila jitihada zinazofanywa katika kufikia malengo fulani huwa hakukosi changamoto. Katika jitihada za kufanya Kiswahili kuwa lugha ya kiteknolojia kumetokea changamoto nyingi, moja wapo iliyo kuu kabisa ni kwamba lugha ya Kiswahili haimilikiwi na taifa lolote tajiri kwa hiyo katika harakatika za kuendeleza inakumbana na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa fedha na hata utayari wa viongozi wa kisiasa kukiendeleza Kiswahili ni mdogo sana, hata hivyo harakati hizi zinapingwa na mataifa ambayo lugha zao zimeendelea sana kiteknolojia kwa kuhofia kwamba zitafunikwa na matumizi ya Kiswahili. Wapo tayari kutoa misaada ili kuendeleza lugha zao kukididimiza Kiswahili kitu ambacho kinafanya harakati za kukiendeleza Kiswahili kuwa ngumu kwani nchi kinamozungumzwa Kiswahili hazina pesa za kupambana na mataifa makubwa yanayopigia upatu lugha zao. Kutokana na sababu hizo, kasi ya uundaji wa istilahi za kiteknolo...
Maoni
Chapisha Maoni