Ndugu Mpendwa kwa pamoja Tunakukaribisha sana katika
Safu hii Fahamu yakwamba Tupo hapa kwaajili yako na kwa
msaada zaidi wa Ushahuri au Maombezi ya mahitaji mbali
mbali Masaa 24 siku 7 za wiki, Piga No:
0756809209/0786608801/0653294219 Itapokelewa na
Mtumishi wa Mungu mwenyewe Samson mboya,
Calivary
Assemblies of
God - Geita
Nyankumbu-
(Hema ya
kinabii )
Newer Post Older Post Home
NENO LA MUNGU LINA NENA NINI JUU YA
USHOGA?
Je, Neno la Mungu lina nena nini juu ya ushoga ? Je, ni(
dhambi?)
Biblia inasisitiza kila mara kwamba ushoga ni dhambi
(mwanzo 19:1-13; mambo ya walawi 18: 22; warumi
1:26-27; wakorintho wa kwanza 6:9). Warumi 1:26-27
inatufundisha ya kwamba ushoga ni njia mojawapo ya
kumkana na kutomtii Mungu. Mtu anapodumu katika dhambi
na kutokuamini biblia inatuambia ya kwamba “Mungu
huwaachilia” kutenda maovu zaidi ili wapate kujua ubatili wa
maisha bila Uwepo wa Mungu. Wakorintho wa kwanza 6:9
inasema kuwa mashoga hawataurithi ufalme wa Mungu.
Mungu haumbi mwanadamu mwenye tamaa ya ushoga.
Biblia inatuambia mtu huwa shoga kwa sababu ya dhambi.
(warumi 1:24-27), na pia kwa sababu ya uamuzi wake
mwenyewe. Mtu anaweza kuzaliwa na msukumo juu ya
ushoga
kama vile watu pia huzaliwa na msukumo juu ya
fujo na dhambi nyinginezo. Hili halihalalishi dhambi yoyote
inayofanywa na wanadamu. Je, mtu akizaliwa na msukumo
wa hasira mbaya, ni halali aendeleze hasira zake mbaya? La,
hasha. Hata kwa ushoga pia si halali.
Hata hivyo Biblia haiitaji dhambi ya ushoga kuwa ndiyo
kubwa zaidi. Kila dhambi ni chukizo kwa Mungu. Ushoga ni
mojawapo ya mambo yaliyoorodheshwa katika wakorintho
wa kwanza 6:9-10 yatakayozuia mtu asiingie katika ufalme
wa Mungu. Kulingana na Biblia msamaha wa Mungu juu ya
shoga upo sawa na wa mzinzi, muabudu sanamu, muuaji,
mwizi na kadhalika. Mungu tena aahidi uwezo juu ya
kushinda dhambi, pamoja na ushoga , kwa wale wote
watakao mwaminiYesu kristo kwa wokovu wao (wakorintho
wa kwanza 6:11; wakorintho wa pili 5:17).
Sina maana ya kufuatilia maisha ya mtu lah! Bali ni mimi
ninatumika tu kufikisha ujumbe kwa jamii yetu na nina amini
hata mashoga matatembelea hii Safu bila shaka itanamsaidia
mwenye tabia hii ya ushoga kuiacha mara moja
,japo wapo wengine ambao sijazungumzia sana
hapa ila watakuwa wameelezewa ukurasa mwingine wale
wanao lawiti, watoto,wadogo,wake zao au wake za watu
wengine kwa yeyote anayefanya tendo hili ni vema kama
ulikuwa haufahamu fahamu sasa kuwa unafanya chukizo
mbele ya uso wa Mungu, acha mara moja na utubu kabisa,
MAOMBI YA MWENYE THAMBI : Ombi la mwenye dhambi ni gani?" Ombi la mwenye dhambi ni Ombi ambalo mtu huomba kwa Mungu wakati anapotambua ya kwamba yeye ni mwenye dhambi au ametenda thambi na anahitaji kusamehewa na Mwokozi. Kusema Ombi hili la mwenye dhambi haikamilishi tayari kila kitu. Ombi la mwenye dhambi hufanya kazi tu sawasawa linapokuwa limesimamia kile mtu anacho fahamu, anacho elewa, na kukubali kuhusu dhambi zake na hitaji la Wokovu. Hatua ya kwanza ya Ombi la mwenye dhambi ni kufahamu ya kwamba sisi sote ni wenye dhambi. Warumi 3:10 , “Kama ilivyoandikwa,ya kwamba,Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Bibilia inaonyesha wazi ya kwamba sisi sote tumefanya dhambi. Sisi sote ni wenye dhambi na tunahitaji rehema na msamaha toka kwa Mungu (Tito 3:5-7). Kwa ajili ya dhambi zetu,tunastahili adhabu ya milele (Mathayo 25:46). Ombi hili la mwenye dhambi ni kwa kutafuta neema badala ya hukumu. Ni ombi la kuulizia rehema badala ya hasira kuu.rehema ni kuhesabiwa ...
Maoni
Chapisha Maoni