Serikali wilayani Mkinga imeandaa operesheni maalum ya kukamata baadhi ya wafanyabishara wa nchi jirani ya Kenya kwa kushirikiana na wale wa hapa nchini kufuatia baadhi yao kuingia katika maeneo ya hifadhi kisha kuvuna misitu ya miti aina ya Mikarambati kinyume cha sheria.
Akizungumza na mwandishi wetu wilayani Mkinga baada ya operesheni iliyofanywa awali kufanikiwa lakini baadhi ya wahamiaji kutoka nchi jirani ya Kenya wameanza kuingia kupitia njia za majini na njia za panya mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mboni Mgaza amesema hatua hiyo inafuatia misitu ya hifadhi kuharibiwa vibaya katika baadhi ya maeneo na kupoteza uoto wa asili.
Kwa upande wake afisa misitu wilayani Mkinga Bwana Frank Chambo akielezea uharibifu wanaoufanya baadhi ya wageni kutoka nchi jirani ya Kenya amesema wanakata miti ya hifadhi aina ya Mikarambato kwa ajili ya kutengeneza vinyago huku wengine wakikata miti aina ya Mikoko ambayo inazuia nguvu ya maji ya bahari yasiweze kuvunja kingo za bahari ya Hindi na kusababisha madhara kwa jamii.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Mkinga Mboni Mgaza amesema wilaya yake imeanza ukaguzi maalum wa nyumba hadi nyumba na shule zote za msingi na sekondari kwa ajili ya kukagua baadhi ya watu na taasisi ambazo hazina vyoo ikiwa ni hatua ya kudhibiti magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu.
Changamoto zinazoikabili lugha ya Kiswahili katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Kila jitihada zinazofanywa katika kufikia malengo fulani huwa hakukosi changamoto. Katika jitihada za kufanya Kiswahili kuwa lugha ya kiteknolojia kumetokea changamoto nyingi, moja wapo iliyo kuu kabisa ni kwamba lugha ya Kiswahili haimilikiwi na taifa lolote tajiri kwa hiyo katika harakatika za kuendeleza inakumbana na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa fedha na hata utayari wa viongozi wa kisiasa kukiendeleza Kiswahili ni mdogo sana, hata hivyo harakati hizi zinapingwa na mataifa ambayo lugha zao zimeendelea sana kiteknolojia kwa kuhofia kwamba zitafunikwa na matumizi ya Kiswahili. Wapo tayari kutoa misaada ili kuendeleza lugha zao kukididimiza Kiswahili kitu ambacho kinafanya harakati za kukiendeleza Kiswahili kuwa ngumu kwani nchi kinamozungumzwa Kiswahili hazina pesa za kupambana na mataifa makubwa yanayopigia upatu lugha zao. Kutokana na sababu hizo, kasi ya uundaji wa istilahi za kiteknolo...
Maoni
Chapisha Maoni