SAKATA la wafanyabiashara watano waliogoma kulipa kodi ndani ya muda uliowekwa na Rais John Magufuli limechukua sura mpya baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwakabidhi kwenye vyombo vya dola kwa hatua za kisheria.
Wafanyabiashara hao ni miongoni mwa 43 ambao awali walitajwa kupitisha makontena 329 bandarini bila kuyalipia kodi.
Mwishoni mwa mwaka jana, Rais Magufuli alitoa siku saba wajisalimishe wenyewe kulipa kodi kwa TRA bila adhabu.
Akizungumza na Nipashe ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA, Richard Kayombo alisema kutokana na muda uliotolewa kuisha na wafanyabiashara hao kushindwa kutekeleza walichoagizwa vyombo vya dola vinaendelea kulifanyia kazi suala hilo ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Alisema wameamua kuvishirikisha vyombo vya dola kwa sababu wafanyabiashara hao wamekiuka agizo lililotolewa awali la kuwataka walipe kodi kwa hiyari yao ndani ya muda waliopewa.
Alisema makampuni ya wafanyabiashara hao, matatu yalichukua makadirio ya kodi wanayodaiwa na serikali lakini hayakwenda kulipa na mawili hayakuchukua kabisa.
Alisisitiza kuwa mpaka sasa fedha ambazo zimeshalipwa ni zaidi ya Sh. bilioni 11.9 ambapo wapo waliolipa zote na wengine kulipa sehemu ya malipo.
“Wafanyabiashara 19 wamelipa fedha zote walizokuwa wanadaiwa na wengine 19 wamelipa sehemu ya malipo, lakini wengine wamegoma wanahoji kulipa sehemu za adhabu,” alisema. “Mazungumzo yanaendelea kuhusu wafanyabiashara hao.”
Mwishoni mwa mwaka jana, Rais Magufuli alitoa siku saba kwa wafanyabiashara hao kulipa kodi na kwamba mara baada ya muda huo kupita hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Makontena hayo yaliondolewa bila kulipiwa kodi katika Bandari Kavu kadhaa, ikiwemo ya Azam inayomilikuwa na mfanyabiashara Said Salim Bakhresa.
MAOMBI YA MWENYE THAMBI : Ombi la mwenye dhambi ni gani?" Ombi la mwenye dhambi ni Ombi ambalo mtu huomba kwa Mungu wakati anapotambua ya kwamba yeye ni mwenye dhambi au ametenda thambi na anahitaji kusamehewa na Mwokozi. Kusema Ombi hili la mwenye dhambi haikamilishi tayari kila kitu. Ombi la mwenye dhambi hufanya kazi tu sawasawa linapokuwa limesimamia kile mtu anacho fahamu, anacho elewa, na kukubali kuhusu dhambi zake na hitaji la Wokovu. Hatua ya kwanza ya Ombi la mwenye dhambi ni kufahamu ya kwamba sisi sote ni wenye dhambi. Warumi 3:10 , “Kama ilivyoandikwa,ya kwamba,Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Bibilia inaonyesha wazi ya kwamba sisi sote tumefanya dhambi. Sisi sote ni wenye dhambi na tunahitaji rehema na msamaha toka kwa Mungu (Tito 3:5-7). Kwa ajili ya dhambi zetu,tunastahili adhabu ya milele (Mathayo 25:46). Ombi hili la mwenye dhambi ni kwa kutafuta neema badala ya hukumu. Ni ombi la kuulizia rehema badala ya hasira kuu.rehema ni kuhesabiwa ...
Maoni
Chapisha Maoni