Shetani yuko duniani, na anafanya kazi duniani. Watu wengi wanapokua wanapambana na shetani wanakua wanawaza kwamba yuko mbali sana na wao.
Shetani amewakilishwa na majina mbali mbali katika biblia; mfano
> Shetani
> Ibilisi
> Mwovu
Shahidi nane kibiblia zinazoonyesha shetani anakaa duniani.
1. Shetani alitupwa duniani
Ufunuo 12:12
2. Shimo la kuzimu lipo hapa hapa duniani
Ufunuo 9:1-2,11
3. Siku moja alionekana duniani anazunguka zunguka.
Ayubu 1:7, ayubu 2:2
Shetani anazunguka zunguka na pia anatembea tembea. Hivyo unaweza kukutana nae anatembea, au anazunguka zunguka.
Bwana aliongea na shetani ili sisi tuweze kujifunza kutoka Kwenye maongezi yake.
4. Shetani aligombania mwili kwenye mazishi.
Kumbu 34:1-6 Hapa biblia inaonyesha Musa amekufa,na Mungu akamzika.
Lakini Yuda 1:9 shetani akashindana na mikaeli kwa ajili ya mwili wa Musa.
5. Shetani aliingia kwenye ibada wakati Kuhani mkuu Yoshua akiendesha ibada
Zekaria 3:1-2
6. Shetani aliongea na Daudi.
1 Nyakati 21:1
7. Dunia yote inakaa katika yule mwovu.
1 Yohana 5:19.
8. Shetani anaitwa Mungu aw dunia hii
2 Wakorintho 4:4
USHAHIDI KUWA SHETANI ANA SERIKALI YAKE.
katika agano la kale, mkuu wa nchi alikuwa ni mfalme, na ndio sababu hata shetani anajiita mfalme, kuonyesha Kuwa anautawala wake. Kwa hiyo kwa Leo angeweza kuitwa rais. Ni mkuu aw ulimwengu, maana yake Ana SERIKALI yake hapa ulimwenguni.
Yohana 12:31.
Shetani anaitwa Lusifa, maana yake mtoa mwanga, au nuru. Ndio maana mtu anayefanya mambo ya kishetani unaona anafanikiwa, ni kwasababu shetani anawapa nuru ya kufanikiwa katika uovu wake.
Ameitwa mkuu wa Ulimwengu.
Yohana 14:3, Yohana 16:11
Kwahiyo kwakua ni mkuu wa ulimwengu, anakua ni utawala wake au serikali yake.
Sehemu nyingine anaitwa baba wa uongo. Neno baba maana yake sio mwanaume, Mungu anaitwa baba na sio mwanamke wala mwanaume.
Neno baba maana yake ni muanzilishi au asili ya..
Shetani anapoitwa baba aw uongo, maana yake ni muanzilishi au ndie asili ya uongo.
Yohana 8:44
Shetani ana watoto waliochini yake, Kama ambavyo Mungu anazaa, shetani nae anazaa. Kama ambavyo asili yake ni uasi, uongo na ushetani yeye naye huzaa watoto wa jinsi yake.
1 Yohana3:1
MUUNDO WA SERIKALI YA KISHETANI.
Serikali ya kishetani imejengwa kijeshi zaidi, tofauti na serikali nyingine duniani ambazo zimejengwa kiraia
Serikali ya shetani imezaliwa kivita baada ya kupigana toka mbinguni.
Waefeso 6:12
Tunapambana na:-
Falme: falme maana yake baada ya shetani kuna wafalme wengine ambao nao ni Wakuu.
Hawa ni wafalme ambao sio shetani mwenyewe Bali ni wawakilishi aw shetani ,
Mamlaka: hizi ni idara mbali mbali zilipo kwaajili ya kutimiza makusudi ya kishetani.
Luka 8:28-30
Mashetani wanaulizwa wao ni akina nani? Wanajibu wao ni Jeshi maana tuko wengi
SERIKALI YA SHETANI IMEGAWANYIKA KATIKA SEHEMU KUBWA MBILI.
1) Wale wanaotenda kazi rohoni, wanashambulia kutokea rohoni. Hawa ndio wanaoshambulia ndotoni na mapepo wanao wanavaa watu.
2) Wale wanaotenda kazi wakiwa mwilini. Hawa wanavaa miili ili kutenda kazi katika mwili.
Malaika walikwenda kwa Abraham walionekana Kama watu., walienda kwa Lutu wakaonekana Kama watu, na watu wa mji wakataka Kuwaoa.
Uthibitisho wa mashetani kuvaa miili.
Imeandikwa :Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? (MT. 3:7 SUV)
Imeandikwa : Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. (MT. 12:34 SUV)
Imeandikwa :Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea ili awabatize, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? (LK. 3:7 SUV)
Yesu alipokea mamlaka kutoka. Kwa Baba wa mbinguni , na moja ya kazi yake ilikua ni kubatilisha nguvu za giza zote na mamlaka yote. Ndio sababu kazi ya kanisa ni kuzibatilisha kazi za shetani zote ili Yesu aje kulichukua kanisa
Imeandikwa : Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. (1 KOR. 15:24 SUV)
SHETANI ANATAWALA MAENEO MAKUU MATATU( sub headquarter)
1. Majini
2. Angani
3. Nchi kavu.
Kwanini shetani amekua kufanya makao yake katika maeneo haya?
Ni kwasababu maeneo hayo ndio maeneo ya kutawala na kumiliki, unapokea katika maeneo hayo inakupa kumiliki na kutawala. Ndio sababu Adamu alikuwa hivyo ili atawale.
Imeandikwa :Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. (MWA. 1:26 SUV)
Ni naamuru kwa jina la Yesu, kila eneo la maisha yako lililoshikiliwa na shetani liachiliwe, Mungu na akupe kutiisha, kumiliki na kutawala 2015 kwa Jina la Yesu.
MAOMBI YA MWENYE THAMBI : Ombi la mwenye dhambi ni gani?" Ombi la mwenye dhambi ni Ombi ambalo mtu huomba kwa Mungu wakati anapotambua ya kwamba yeye ni mwenye dhambi au ametenda thambi na anahitaji kusamehewa na Mwokozi. Kusema Ombi hili la mwenye dhambi haikamilishi tayari kila kitu. Ombi la mwenye dhambi hufanya kazi tu sawasawa linapokuwa limesimamia kile mtu anacho fahamu, anacho elewa, na kukubali kuhusu dhambi zake na hitaji la Wokovu. Hatua ya kwanza ya Ombi la mwenye dhambi ni kufahamu ya kwamba sisi sote ni wenye dhambi. Warumi 3:10 , “Kama ilivyoandikwa,ya kwamba,Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Bibilia inaonyesha wazi ya kwamba sisi sote tumefanya dhambi. Sisi sote ni wenye dhambi na tunahitaji rehema na msamaha toka kwa Mungu (Tito 3:5-7). Kwa ajili ya dhambi zetu,tunastahili adhabu ya milele (Mathayo 25:46). Ombi hili la mwenye dhambi ni kwa kutafuta neema badala ya hukumu. Ni ombi la kuulizia rehema badala ya hasira kuu.rehema ni kuhesabiwa haki
Maoni
Chapisha Maoni