Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2015
November 14, 2015 Mambo yameanza Dodoma, ratiba ya Bunge ni hii + pichaz Wabunge waliofika.. Newsroom TZA Kama umetembelea mitandao ya kijamii utakuwa umeona pilikapilika za kinachoendelea Dodoma sasahivi, baada ya Uchaguzi Mkuu kuisha wale wote waliopita kwenye nafasi ya Ubunge wanasubiri shughuli ya kuapishwa halafu Vikao vya Bunge vinaanza. Nimeipata Ratiba ya kitakachoendelea Dodoma kwa jumla ya siku saba mfululizo, yani kuanzia jana November 13 mpaka November 20 2015… Ratiba yenyewe hii hapa. Mbunge Mteule wa Jimbo Mwanga K’njaro, Prof. Jumanne Maghembe akiwasilisha nyaraka zake wakati wa kusajiliwa Bungeni Dodoma. Mbunge Mteule wa Sengerema, William Ngeleja nae kwenye foleni ya usajili katika Viwanja vya Bunge Dodoma

HARUFU MBAYA MDOMONI

Chanzo cha harufu mbaya mdomoni http://www.MAHANAIMU. Blog /2015/11/chanzo-cha-harufu-mbaya-mdomoni.html
TAARIFA YA MH EDWARD NGOYAI LOWASSA KWA VYOMBO YVA HABARI JUU YA HALI YA KISIASA NCHINI http://www.muungwana.com/2015/11/taarifa-ya-mh-edward-ngoyai-lowassa-kwa.html
A TO Z YA KIFO CHA KIGOGO WA CHADEMA MKOA NA MBINU ILIYOTUMIKA KUMUA KINYAMA GEITA NDIVYO ILIVYOKUWA HIVI. http:// mahanaimu. Com /2015/11/a-to-z-ya-kifo-cha-kigogo-wa-chadema.html

CHADEMA HAIKUBALIANI NA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU 2015

WAKATI  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ikimtangaza  mshindi wa urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Jumapili iliyopita, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeyakataa matokeo hayo. Kimesema hakitakubali matokeo ya urais yatakayotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa madai kuwa mchakato wa kuhesabu kura umekiukwa na haukufuata sheria. Aidha, chama hicho kimetaka NEC kusimamisha kutangaza matokeo hayo kwa kuwa yako kinyume cha utaratibu. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa alidai utangazaji wa matokeo hayo umevurugwa na watendaji wa tume hiyo ili kukisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM). “Katika maeneo mengi ambako matokeo yameshatangazwa mpaka sasa, kilichoripotiwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais, hakifanani wala kuendana na matakwa halisi ya wananchi. Matokeo mengi yamesheheni udanganyifu, ulaghai na yameandaliwa kwa lengo maalumu la kumbeba mgombea wa CCM, John Pombe...

MAGUFULI ATAKIWA KUZUIA UNYWAJI WA POMBE WAKAZI WA KAZI

WAKAZI wa Jiji la Arusha wamemtaka Rais Mteule, Dk John Magufuli kuhakikisha anasimamia utekelezaji na uwajibikaji kwa kila Mtanzania na kupiga vita baa na vijiwe vya kahawa kufunguliwa wakati wa kazi. Mmoja wa wakazi wa Jiji la Arusha anayeishi Moshono, Julius Mollel alisema kuwa katika miaka ya 1970 hadi 1980 sehemu zote za starehe zikiwemo baa na vijiwe vya kahawa vilikuwa vikifunguliwa baada ya kazi. Mollel alisema nyakati hizo wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa jiji na halmashauri walikuwa mstari wa mbele kusimamia sheria hiyo na kila mtu alikuwa akiwajibika kwa kufanya kazi bila kusukumwa. Alisema kwa sasa inashangaza kuona Jiji la Arusha toka asubuhi baa na maduka ya pombe yako wazi. Katika vijiwe vya kahawa watu wamejaa wanazungumza siasa na kushindwa kufanya kazi na kubaki kulalamika hovyo hovyo. ‘’Ninamwomba Magufuli awaagize watendaji wa serikali ngazi ya Jiji, Wilaya na Mkoa kusimamia sheria za muda wa kazi kufanya kazi na kua...

MSEMAJI MKUU WA SERIKAKALI AFAFANUA JUU YA MAENEO YALIOENEA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU MKAPA

Wednesday, November 4, 2015 Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana ) Mpekuzi blog Serikali Yakanusha Taarifa za Kifo cha Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Assah Mwambene amekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kuwa amefariki Dunia. Akizungunza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mwambene amesema Rais Mkapa yupo salama na mzima wa afya na hakuna maradhi yoyote yanayomsumbua. Mwambene amewaasa watumiaji wa mitandao mbalimbali hasa Blogs kuacha kuitumia mitandao hiyo kwa kupotosha umma na kuandika nambo yasiyo na ukweli ili kuepusha mifumuko ya habari za upotishaji. “Si jambo jema na wanaofanya hivyo waache mara moja kabla ya hatua stahiki hazijachukuliwa,” amesema Mwambene. Amesema kuwa jambo la kumzushia mtu kifo si jambo zuri ambalo amelizungumza kama ‘uchuro’ kwa mtu husika na kumtabiria mabaya. “Mkapa yupo hai n...