WAKAZI wa Jiji la Arusha wamemtaka Rais
Mteule, Dk John Magufuli kuhakikisha anasimamia
utekelezaji na uwajibikaji kwa kila Mtanzania na
kupiga vita baa na vijiwe vya kahawa kufunguliwa
wakati wa kazi.
Mmoja wa wakazi wa Jiji la Arusha anayeishi
Moshono, Julius Mollel alisema kuwa katika miaka
ya 1970 hadi 1980 sehemu zote za starehe
zikiwemo baa na vijiwe vya kahawa vilikuwa
vikifunguliwa baada ya kazi.
Mollel alisema nyakati hizo wakuu wa mikoa,
wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa jiji na
halmashauri walikuwa mstari wa mbele kusimamia
sheria hiyo na kila mtu alikuwa akiwajibika kwa
kufanya kazi bila kusukumwa.
Alisema kwa sasa inashangaza kuona Jiji la
Arusha toka asubuhi baa na maduka ya pombe
yako wazi. Katika vijiwe vya kahawa watu wamejaa
wanazungumza siasa na kushindwa kufanya kazi
na kubaki kulalamika hovyo hovyo.
‘’Ninamwomba Magufuli awaagize watendaji wa
serikali ngazi ya Jiji, Wilaya na Mkoa kusimamia
sheria za muda wa kazi kufanya kazi na kuacha
kunywa pombe,‘’ alisema.
Naye Peter Massawe alisema kuwa uzembe uliopo
kwa watendaji wa serikali katika jiji na halmashauri
kwa kushindwa kusimamia sheria hiyo ndio
umefanya Arusha watu kuanza kunywa pombe
kuanzia asubuhi.
Massawe ambaye ni mkazi wa Sanawari alisema
kuwa wakazi wa Arusha wameshazoea kunywa
pombe kuanzia asubuhi na sasa wanaona kama ni
haki yao kufanya hivyo wakati hilo ni kosa.
Alisema kuwa enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere, sehemu zote za starehe zilikuwa
zikiruhusiwa kufunguliwa baada ya saa 8:00
mchana na muda wote watu wanatakiwa kufanya
kazi na sio kukaa baa.
Juma Masoud mkazi wa kata ya Kati alisema
inasikitisha kuona wakazi wa Arusha kucha kutwa
wanakunywa pombe na kunywa kahawa kuanzia
asubuhi.
Masoud alisema wala rushwa wamejaa katika
halmashauri na jiji na kushindwa kusimamia hilo
hivyo Magufuli anapaswa kuwawajibisha
wanaoshindwa kusimamia sheria ya kufanya kazi
na kuacha watu wakinywa pombe asubuhi.
Changamoto zinazoikabili lugha ya Kiswahili katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Kila jitihada zinazofanywa katika kufikia malengo fulani huwa hakukosi changamoto. Katika jitihada za kufanya Kiswahili kuwa lugha ya kiteknolojia kumetokea changamoto nyingi, moja wapo iliyo kuu kabisa ni kwamba lugha ya Kiswahili haimilikiwi na taifa lolote tajiri kwa hiyo katika harakatika za kuendeleza inakumbana na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa fedha na hata utayari wa viongozi wa kisiasa kukiendeleza Kiswahili ni mdogo sana, hata hivyo harakati hizi zinapingwa na mataifa ambayo lugha zao zimeendelea sana kiteknolojia kwa kuhofia kwamba zitafunikwa na matumizi ya Kiswahili. Wapo tayari kutoa misaada ili kuendeleza lugha zao kukididimiza Kiswahili kitu ambacho kinafanya harakati za kukiendeleza Kiswahili kuwa ngumu kwani nchi kinamozungumzwa Kiswahili hazina pesa za kupambana na mataifa makubwa yanayopigia upatu lugha zao. Kutokana na sababu hizo, kasi ya uundaji wa istilahi za kiteknolo...
Maoni
Chapisha Maoni