Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameombwa kufuta hati ya shamba la mwekezaji katika Kijiji cha Kenyana Kata ya Ring’wani wilayani hapa Mkoa wa Mara kwa madai ya kushindwa kuliendeleza.
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara na diwani wa kata hiyo, Maiso Mahemba, wakazi wa kijiji hicho walidai eneo hilo ambalo limechukuliwa na mwekezaji huyo miaka 29 iliyopita, linatakiwa kubatilishwa matumizi kutoka uwekezaji ili liwe na umma.
Walisema ni vema Serikali ikawaruhusu wajenge shule ya msingi kwa ajili ya watoto wao ambao hawajaanza masomo.
Mmoja wa wakazi hao, Enock Magoiga alisema: “Mwekezaji huyo ana faida gani kwa wananchi kama amechukua eneo halafu hajawahi kuonekana wala kuliendeleza. Tunazuiwa kufanya maendeleo bila sababu za msingi, tunaomba Waziri William Lukuvi afute hati hiyo.”
Alisema mazingira hayo yamechangia shule waliyojenga kukataliwa kufunguliwa kwa madai kuwa wamejenga kwenye eneo la mwekezaji na kwamba matokeo yake watoto wao zaidi ya 800 wengi wakiwa na umri zaidi ya miaka 12, hawajaanza masomo.
Diwani Mahemba alisema tangu mwaka 1992 wakazi hao waliingia katika eneo hilo kwa kupokelewa na Serikali na kuanza kujenga makazi yao.
Alisema baadaye walitambuliwa na kupewa kitongoji hicho, kwa kutumia nguvu zao waliamua kujenga shule hiyo, lakini imezuiwa kufunguliwa kwa misingi ya ubaguzi wa kikabila.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kenyana, Matiko Nsaho alithibitisha kuwa eneo hilo lina hati ya muda mrefu na linamilikiwa na raia wa Finland ambaye kwa sasa ni marehemu.
Kaimu Ofisa Elimu Wilaya hiyo, Wanyancha Nyakoge alisema waraka namba 5 wa Mwaka 2015 kupitia mwongozo wa utekelezaji unaagiza maeneo ambayo yako mbali na shule wanatakiwa kuanzisha shule shinikizi kuanzia darasa la awali hadi darasa la pili.
Changamoto zinazoikabili lugha ya Kiswahili katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Kila jitihada zinazofanywa katika kufikia malengo fulani huwa hakukosi changamoto. Katika jitihada za kufanya Kiswahili kuwa lugha ya kiteknolojia kumetokea changamoto nyingi, moja wapo iliyo kuu kabisa ni kwamba lugha ya Kiswahili haimilikiwi na taifa lolote tajiri kwa hiyo katika harakatika za kuendeleza inakumbana na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa fedha na hata utayari wa viongozi wa kisiasa kukiendeleza Kiswahili ni mdogo sana, hata hivyo harakati hizi zinapingwa na mataifa ambayo lugha zao zimeendelea sana kiteknolojia kwa kuhofia kwamba zitafunikwa na matumizi ya Kiswahili. Wapo tayari kutoa misaada ili kuendeleza lugha zao kukididimiza Kiswahili kitu ambacho kinafanya harakati za kukiendeleza Kiswahili kuwa ngumu kwani nchi kinamozungumzwa Kiswahili hazina pesa za kupambana na mataifa makubwa yanayopigia upatu lugha zao. Kutokana na sababu hizo, kasi ya uundaji wa istilahi za kiteknolo...
Maoni
Chapisha Maoni