Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUONDOA VIRUSI KWENYE SIMU ZETU

Unapogundua simu yako ya Android smartphone imeingiliwa na virus ni vizuri kuhakikisha unaondoa haraka ili kupunguza hatari ya data zako kwenye simu kuharibiwa au kupotea kabisa. 

Hapa nataka kukuelekeza jinsi ya kuondoa virus kwenye simu yako ya Android smartphone. 

Kama unafikiri au umegundua kuwa simu yako imeingiliwa na virus, moja kati ya  free antivirus programs kwa ajili ya simu za Android ni: AVG AntiVirus.

1. kitu cha kwanza kufanya ni kupakua (download) na ku-install AVG Antivirus kutoka Google Play  au INGIA HAPA

2.Baada ya kuwa umekubali (accepted)  permissions, umepakua (download) na ku-install hiyo application,  ifungue. Activate application na  click kwenyeProtection option.

3.Halafu, kwenye orodha ya options, click kwenye "Scan Now". Application itaanza ku-scan mafaili yote yaliyomo kwenye simu yako.

4.Antivirus hii itatafuta viruses na malware ambao wapo kwenye simu yako ya Android smartphone au tablet na baada ya kumaliza itawatoa virus wote.

5. Ili kuhakikisha simu yako inakuwa kwenye usalama siku zote unashauriwa kuendesha (run)  antivirus mara moja kwa wiki. Na ni vizuri kutumia antivirus hii wakati simu yako ikiwa imeunganishwa kwenye power supply yaani ikiwa kwenye chaji au ikiwa na chaji fully.

 Hii ndio njia ya haraka na yenye ufanisi kusafisha na kulinda simu yako ya android smartphone isidhurike na virus.

Maoni

  1. Nipende kushukuru kwa maelezo mazuri napenda kuyafanyia kazi coz cm yangu inanisumbua sana.....

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHANGAMOTO KATIKA LUGHA YA KISWAHILI KWENYE MAMBO YA KOMPYUTA (TEHAMA)

Changamoto zinazoikabili lugha ya Kiswahili katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Kila jitihada zinazofanywa katika kufikia malengo fulani huwa hakukosi changamoto. Katika jitihada za kufanya Kiswahili kuwa lugha ya kiteknolojia kumetokea changamoto nyingi, moja wapo iliyo kuu kabisa ni kwamba lugha ya Kiswahili haimilikiwi na taifa lolote tajiri kwa hiyo katika harakatika za kuendeleza inakumbana na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa fedha na hata utayari wa viongozi wa kisiasa kukiendeleza Kiswahili ni mdogo sana, hata hivyo harakati hizi zinapingwa na mataifa ambayo lugha zao zimeendelea sana kiteknolojia kwa kuhofia kwamba zitafunikwa na matumizi ya Kiswahili. Wapo tayari kutoa misaada ili kuendeleza lugha zao kukididimiza Kiswahili kitu ambacho kinafanya harakati za kukiendeleza Kiswahili kuwa ngumu kwani nchi kinamozungumzwa Kiswahili hazina pesa za kupambana na mataifa makubwa yanayopigia upatu lugha zao. Kutokana na sababu hizo, kasi ya uundaji wa istilahi za kiteknolo...

MAOMBI YA MWENYE DHAMBI

MAOMBI YA MWENYE THAMBI : Ombi la mwenye dhambi ni gani?" Ombi la mwenye dhambi ni Ombi ambalo mtu huomba kwa Mungu wakati anapotambua ya kwamba yeye ni mwenye dhambi au ametenda thambi na anahitaji kusamehewa na Mwokozi. Kusema Ombi hili la mwenye dhambi haikamilishi tayari kila kitu. Ombi la mwenye dhambi hufanya kazi tu sawasawa linapokuwa limesimamia kile mtu anacho fahamu, anacho elewa, na kukubali kuhusu dhambi zake na hitaji la Wokovu. Hatua ya kwanza ya Ombi la mwenye dhambi ni kufahamu ya kwamba sisi sote ni wenye dhambi. Warumi 3:10 , “Kama ilivyoandikwa,ya kwamba,Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Bibilia inaonyesha wazi ya kwamba sisi sote tumefanya dhambi. Sisi sote ni wenye dhambi na tunahitaji rehema na msamaha toka kwa Mungu (Tito 3:5-7). Kwa ajili ya dhambi zetu,tunastahili adhabu ya milele (Mathayo 25:46). Ombi hili la mwenye dhambi ni kwa kutafuta neema badala ya hukumu. Ni ombi la kuulizia rehema badala ya hasira kuu.rehema ni kuhesabiwa ...

YESU NI NANI.

Kuna maswali mengi sana unopo mtaja yesu ila naomba ufuatane pamoja nami hatua moja hadi nyingile ili tumjue yesu ni nani k aribia miaka 2.000 iliyopita Yesu aliwauliza wanafunzi wake maswali maswali mawili ambayo mpaka sasa yamo ndani ya Mioyo na fikra za wanaadamu 1." watu hunena kuwa mwana wa adamu kuwa ni nani ?" 2. na ninyi mwanena mm kuwa ni nani ?" matayo .16:13-16 watu wengi,dini nyingi na hata wasomi wengi(ma-filosofa)wamejaribu kutoa majibu kadhaa  katika kujibu swali la kwanza .baadha ya watu wengine walijibu kuwa yu nabii , na kwa wengine yesu alikuwa mwalimu mkuu na bado kwa wengine alikuwa mtu mwema na mwadilifu ambaye mfano wa maisha yake unastahili kuigwa. Lakini jawabu la swali la pili ni muhimu sana.maana katika jawabu la kila mtu binafsi,ndipo pale penye hatima ya milele ( Yohana3 :36 )lakini haina maana na mawazo ya maisha ya wakati huu( Yohana 10:10; wakolosai3 :3-4; wagalatia2 :20) hivyo ba...