Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2015

CUF YATOA TAMKO ZANZIBAR

Kaimu Mkurugenzi wa habari, uenezi na mawasiliano kwa umma Ismail Jussa. Kufuatia taarifa iliyotolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho iliyokutana Zanzibar juzi, tarehe 27 Desemba, 2015, waandishi wengi wa habari wametupigia simu wakitaka kujua Chama Cha Wananchi (CUF) kimepokea vipi taarifa ile. Vikao vya CCM ni vikao vya CCM. Si kawaida yetu kutolea taarifa maamuzi ya vikao vya vyama vyengine. Hata hivyo, tunaelewa ni kwa nini kumekuwepo na shauku ya kusikia CUF inasema nini kwa sababu yale yaliyokuwemo kwenye taarifa hiyo yaligusia pia mazungumzo yanayofanyika Ikulu Zanzibar yanayolenga kupata ufumbuzi wa mgogoro wa uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015. Baada ya kuipitia taarifa ya CCM na mengine yaliyoelezwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar wakati akitoa ufafanuzi wa yale yaliyomo kwenye taarifa hiyo, CUF tunapenda kuwaeleza Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla haya yafuatayo: 1. Taari

SERIKALI KUWABANA MADAKTARI INAOWASOMESHA NJE YA NCHI

Serikali imesema madaktari wote watakaopata nafasi ya kusoma nje ya nchi kwa ufadhili wake, watafanya hivyo kwa kusaini mkataba. Kufanya hivyo kumeelezewa kuwa kutasaidia kuwabana wale wanaohitimu na kutimkia nje ya nchi kwenda kufanya kazi huko. Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalah alipotembelea Manispaa ya Shinyanga. Alisema Serikali imeendelea kuwapoteza madaktari wengi inaowasomesha wanaokimbia kwa madai ya mazingira mabovu ya kufanyia kazi. Wengi wao hukimbilia nchi za Afrika Kusini na Botswana wanakodai kuna mazingira mazuri ya kufanyia kazi. Alisema wanataka kuona wizara inakuwa na madaktari bingwa wa kutosha kulika ilivyo sasa. Awali, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, Fredrick Mlekwa alimwambia naibu waziri huyo kuwa, tatizo kubwa linalokwamisha utendaji kazi wao ni upungufu wa madaktari hospitali hapo. Dk Mlekwa alisema hospitali hiyo ina madaktari bingwa wanne, madaktari wa kawaida 15

LUKUVI AOMBWA KUFUTA HATI YA SHAMBA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameombwa kufuta hati ya shamba la mwekezaji katika Kijiji cha Kenyana Kata ya Ring’wani wilayani hapa Mkoa wa Mara kwa madai ya kushindwa kuliendeleza. Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara na diwani wa kata hiyo, Maiso Mahemba, wakazi wa kijiji hicho walidai eneo hilo ambalo limechukuliwa na mwekezaji huyo miaka 29 iliyopita, linatakiwa kubatilishwa matumizi kutoka uwekezaji ili liwe na umma. Walisema ni vema Serikali ikawaruhusu wajenge shule ya msingi kwa ajili ya watoto wao ambao hawajaanza masomo. Mmoja wa wakazi hao, Enock Magoiga alisema: “Mwekezaji huyo ana faida gani kwa wananchi kama amechukua eneo halafu hajawahi kuonekana wala kuliendeleza. Tunazuiwa kufanya maendeleo bila sababu za msingi, tunaomba Waziri William Lukuvi afute hati hiyo.” Alisema mazingira hayo yamechangia shule waliyojenga kukataliwa kufunguliwa kwa madai kuwa wamejenga kwenye eneo la mwekezaji na kwamba matokeo yake watoto wao zaidi ya 80

MAOMBI YA MWENYE DHAMBI

MAOMBI YA MWENYE THAMBI : Ombi la mwenye dhambi ni gani?" Ombi la mwenye dhambi ni Ombi ambalo mtu huomba kwa Mungu wakati anapotambua ya kwamba yeye ni mwenye dhambi au ametenda thambi na anahitaji kusamehewa na Mwokozi. Kusema Ombi hili la mwenye dhambi haikamilishi tayari kila kitu. Ombi la mwenye dhambi hufanya kazi tu sawasawa linapokuwa limesimamia kile mtu anacho fahamu, anacho elewa, na kukubali kuhusu dhambi zake na hitaji la Wokovu. Hatua ya kwanza ya Ombi la mwenye dhambi ni kufahamu ya kwamba sisi sote ni wenye dhambi. Warumi 3:10 , “Kama ilivyoandikwa,ya kwamba,Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Bibilia inaonyesha wazi ya kwamba sisi sote tumefanya dhambi. Sisi sote ni wenye dhambi na tunahitaji rehema na msamaha toka kwa Mungu (Tito 3:5-7). Kwa ajili ya dhambi zetu,tunastahili adhabu ya milele (Mathayo 25:46). Ombi hili la mwenye dhambi ni kwa kutafuta neema badala ya hukumu. Ni ombi la kuulizia rehema badala ya hasira kuu.rehema ni kuhesabiwa haki

NENO LA UZIMA

Ndugu Mpendwa kwa pamoja Tunakukaribisha sana katika Safu hii Fahamu yakwamba Tupo hapa kwaajili yako na kwa msaada zaidi wa Ushahuri au Maombezi ya mahitaji mbali mbali Masaa 24 siku 7 za wiki, Piga No: 0756809209/0786608801/0653294219 Itapokelewa na Mtumishi wa Mungu mwenyewe Samson mboya, Calivary Assemblies of God - Geita Nyankumbu- (Hema ya kinabii ) Newer Post Older Post Home NENO LA MUNGU LINA NENA NINI JUU YA USHOGA? Je, Neno la Mungu lina nena nini juu ya ushoga ? Je, ni( dhambi?) Biblia inasisitiza kila mara kwamba ushoga ni dhambi (mwanzo 19:1-13; mambo ya walawi 18: 22; warumi 1:26-27; wakorintho wa kwanza 6:9). Warumi 1:26-27 inatufundisha ya kwamba ushoga ni njia mojawapo ya kumkana na kutomtii Mungu. Mtu anapodumu katika dhambi na kutokuamini biblia inatuambia ya kwamba “Mungu huwaachilia” kutenda maovu zaidi ili wapate kujua ubatili wa maisha bila Uwepo wa Mungu. Wakorintho wa kwanza 6:9 inasema kuwa mashoga hawataurithi ufalme wa Mungu. Mung

SERIKALI WILAYANI MKINGA KUWAKAMATA WAHALIFU WANAOVUNA MITI KINYUME NA SHERIA

Serikali wilayani Mkinga imeandaa operesheni maalum ya kukamata baadhi ya wafanyabishara wa nchi jirani ya Kenya kwa kushirikiana na wale wa hapa nchini kufuatia baadhi yao kuingia katika maeneo ya hifadhi kisha kuvuna misitu ya miti aina ya Mikarambati kinyume cha sheria. Akizungumza na mwandishi wetu wilayani Mkinga baada ya operesheni iliyofanywa awali kufanikiwa lakini baadhi ya wahamiaji kutoka nchi jirani ya Kenya wameanza kuingia kupitia njia za majini na njia za panya mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mboni Mgaza amesema hatua hiyo inafuatia misitu ya hifadhi kuharibiwa vibaya katika baadhi ya maeneo na kupoteza uoto wa asili. Kwa upande wake afisa misitu wilayani Mkinga Bwana Frank Chambo akielezea uharibifu wanaoufanya baadhi ya wageni kutoka nchi jirani ya Kenya amesema wanakata miti ya hifadhi aina ya Mikarambato kwa ajili ya kutengeneza vinyago huku wengine wakikata miti aina ya Mikoko ambayo inazuia nguvu ya maji ya bahari yasiweze kuvunja kingo za bahari ya Hin