Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

MATATIZO YA KOMPYUTA

MATATIZO YA IMMA MJUZI KOMPYUTA NA NAMNA YA KUYAEPUKA INSI YA KUTATUA TATIZO HILI LA KUHARIBIKA KWA UBAO MAMA(MOTHERBOARD). 1. Utatuzi wa Shida(troubleshooting), (i) Angalia kama kuna “signal” zinazoonesha kama umeme unaingia kwenye Motherboard, hapa angalia kwenye “Power jeck” kama umeme unaingia kwenye motherboard. (ii) Pima “component” mbalimbali zinazounda mfumo mzima wa ubao mama, moja baada ya nyingine kwa kutumia kifaa kinachoitwa “Multimeter, ukigundua “component” ambayo ni mbovu waweza kuibadilisha. Kabla ya kuibadilisha hiyo “Component” yafaa ukaangalia vitu vifuatavyo; - Uthamani/ufanano wa “component” unazotaka kubadilisha. - Utendaji wa kazi wa “component” hiyo. (iii) Kuibadilisha “component” hiyo. Hapa utaamua kuibadilisha component hiyo kwa kuweka “component” nyingine ambayo ni nzima kama ilivyokuwa mwanzoni. (iv) Fanya usafi kwenye Ubao mama(Motherboard) pamoja na Kompyuta nzima kwa ujumla. (v) Washa Kompyuta yako. 2. Kubadilisha Ubao Mama (Ubao Mama...

CHANGAMOTO KATIKA LUGHA YA KISWAHILI KWENYE MAMBO YA KOMPYUTA (TEHAMA)

Changamoto zinazoikabili lugha ya Kiswahili katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Kila jitihada zinazofanywa katika kufikia malengo fulani huwa hakukosi changamoto. Katika jitihada za kufanya Kiswahili kuwa lugha ya kiteknolojia kumetokea changamoto nyingi, moja wapo iliyo kuu kabisa ni kwamba lugha ya Kiswahili haimilikiwi na taifa lolote tajiri kwa hiyo katika harakatika za kuendeleza inakumbana na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa fedha na hata utayari wa viongozi wa kisiasa kukiendeleza Kiswahili ni mdogo sana, hata hivyo harakati hizi zinapingwa na mataifa ambayo lugha zao zimeendelea sana kiteknolojia kwa kuhofia kwamba zitafunikwa na matumizi ya Kiswahili. Wapo tayari kutoa misaada ili kuendeleza lugha zao kukididimiza Kiswahili kitu ambacho kinafanya harakati za kukiendeleza Kiswahili kuwa ngumu kwani nchi kinamozungumzwa Kiswahili hazina pesa za kupambana na mataifa makubwa yanayopigia upatu lugha zao. Kutokana na sababu hizo, kasi ya uundaji wa istilahi za kiteknolo...

KUROOT SIMU AINA ZOTE

NYUMBANI JINSI YA APPS MUHIMU PAKUA APP YETU Feb 15/2018   10 JINSI YA KUROOT SIMU YAKO HOW TO ROOT YOUR PHONE Nini maana ya kuroot?? Kuroot simu ni kitendo cha kuifanya simu iweze kufanya mambo ambayo hayawezi kufanyika katika mfumo wa kawaida wa android.    Nini faida ya kuroot simu yako? Kubadili mwandiko Kuweka custom ROM Kununua vitu bure katika apps Kufuta app zilizokuja na simu Kuondoa matangazo Kuongeza kasi ya simu Kupunguza matumizi ya battery Hasara za kuroot Kuondoa warranty Hutoweza kupata updates na ukipata hutoweza kuziinstall Uwezekano mkubwa wa kuharibu simu yako JINSI YA KUROOT Kuna njia nyingi za kuroot lakini njia hii nayoenda kukufundisha ndio njia nzuri zaidi! HATUA : Pakua KINGROOT  PAKUA HAPA Hakikisha umeunganishwa na mtandao wa internet Bonyeza "TRY ROOT" nasubiri mpaka itapofika 100% (Simu inaweza kuzima na kuwaka wakati wa hatua hii, ni kitu cha kawaida na hakina madhara yoyote) Baada ya kumalizika utapokea ujumbe"ROOT...

KUONDOA VIRUSI KWENYE SIMU ZETU

Unapogundua simu yako ya Android smartphone imeingiliwa na virus ni vizuri kuhakikisha unaondoa haraka ili kupunguza hatari ya data zako kwenye simu kuharibiwa au kupotea kabisa.  Hapa nataka kukuelekeza jinsi ya kuondoa virus kwenye simu yako ya Android smartphone.  Kama unafikiri au umegundua kuwa simu yako imeingiliwa na virus, moja kati ya   free antivirus programs kwa ajili ya simu za Android ni : AVG AntiVirus. 1. kitu cha kwanza kufanya ni kupakua ( download) na ku-install AVG Antivirus kutoka  Google Play   au  INGIA HAPA 2.Baada ya kuwa umekubali (accepted)  permissions, umepakua (download) na ku-install hiyo application,  ifungue. Activate application na  click kwenye Protection option . 3.Halafu, kwenye orodha ya options, click kwenye " Scan Now ". Application itaanza ku-scan mafaili yote yaliyomo kwenye simu yako. 4.Antivirus hii itatafuta  viruses na malware  ambao wapo kwenye simu yako ya Android smartphone ...

MAHAKA KUU YAIKANA KAMPUNI ILIYOMTOA MBOWE

Mahakama Kuu yaikana kampuni iliyomtoa Mbowe Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe  Dar es Salaam.  Mahakama Kuu imekana kuitambua kampuni ya Fosters Auctioneers and General Traders iliyohusika kuondoa vitu vya kampuni za Freeman Mbowe kwenye jengo la Shirika la Taifa la Nyumba (NHC). Hayo yalibainishwa jana na kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema, Peter Kibatala wakati wa usikilizwaji wa maombi yaliyofunguliwa na mlalamikaji huyo kupitia kampuni ya Mbowe Hotels Ltd dhidi ya NHC na kampuni hiyo ya udalali. Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo jana, pamoja na mambo mengine Mbowe aliiomba Mahakama iliamuru NHC na kampuni hiyo wamrejeshe katika jengo hilo pamoja na vifaa na mali zake zinazoshikiliwa na kampuni hiyo. Wakili Kibatala aliieleza Mahakama kuwa mteja wake aliondolewa katika jengo hilo kinyume na sheria. Alidai dalali aliyetumiwa na NHC kuziondoa kampuni za Mbowe katika jengo hilo hajasajiliwa na Mahakama kwa kuwa wal...

Uchafuzi wa mazingira duniani

92% ya watu duniani wanaishi kwenye hewa chafuzi Uchafuzi wa hali ya hewa Takwimu  mpya za shirika la afya duniani (WHO) kuhusu ubora wa hewa, zimethibitisha kwamba asilimia 92% ya watu duniani wanaishi katika maeneo ambapo viwango vya ubora wa hewa ni vidogo kupita kiasi cha ukomo kilichowekwa na shirika hilo. Kwa mujibu wa shirika hilo takwimu zinatolewa kwa njia ya ramani ambayo inaonesha mahali palipo na hatari ya hewa chafuzi, na kubainisha hatua za msingi za kufuatilia na kukabiliana na hali hiyo. Takribani vifo milioni 3 kila mwaka vinahusishwa na hewa chafuzi hasa nje ya nyumba, lakini shirika hilo linasema hata ile ya ndani husababisha vifo pia. Mwaka 2012 inakadiriwa kwamba vifo milioni 6.5 kote duniani vimetokana na hewa chafuzi ndani na nje ya nyumba huku karibu asilimia 90 ya vifo hivyo vikitokea katika nchi za kipato cha chini na wastani.

WAFUASI WAMTAKA MAALIM AITISHE MKUTANO KUMTAMBUA LIPUMBA

Wafuasi wataka Maalim aitishe mkutano kumtambua Lipumba Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad  Baadhi  ya wafuasi wa aliyekuwa mwenyekiti wa CUF wamesema ili Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad aweze kuingia katika ofisi za makao ya CUF Buguruni ni lazima aitishe mkutano na wanahabari kumtambua Profesa Lipumba. Baadhi ya wafuasi hapo wamekusanyika eneo la ofisi hiyo wakiwa na nia ya kumpokea Profesa Lipumba na kumzuia Maalim Seif endapo atafika. Akizungumza kwa niaba ya wenzake Juma Yassin amesema Maalim Seif ataendelea kubaki Zanzibar iwapo  hatataka kumtambua Profesa Lipumba ambaye ni mwenyekiti halali Kikatiba. "Tumesikia leo huenda akaja lakini ofisi  na asijisumbue tupo tayari kwa lolote hadi amtambue Profesa Lipumba," amesema Yassin ambaye ni mwenyekiti wa Tawi la Kosovo Manzese.

WAZAZI MBARONI KWA KUOZESHA WANAFUNZI

Wazazi mbaroni kwa kuozesha wanafunzi POLISI mkoani Rukwa inawashikilia wazazi watatu, akiwemo mume na mke, kwa kuozesha watoto wao wa kike wenye umri wa miaka 15 waliokuwa wakisoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Chipu katika Kata ya Kasense kwenye Manispaa ya Sumbawanga. Aidha, mmoja wa watoto hao aliyeozeshwa kijijini humo anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano huku mwanamume wake anayedaiwa kuwa ni mtoto wa mwalimu mstaafu, aitwae Daud Kwitwa, akidaiwa kutoroka. Msichana mwingine na mwanamume aliyeozeshwa walitoroka kijijini humo na kwenda katika kitongoji cha Malangali, Manispaa ya Sumbawanga mkoani humo ambapo wanadaiwa kufunga ndoa Agosti katika Kanisa Katoliki la Roho Mtakatifu, Jimbo la Sumbawanga, lililopo kwenye kitongoji cha Malangali. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando, alithibitisha kukamatwa kwa wazazi hao na msichana mmoja, huku Polisi ikiendelea kumsaka msichana mwingine na mumewe. Wazazi waliokamatwa wametajwa kuwa ni Sabastian Sangu na mkewe Hild...

NDALICHAKO APIGWA NA WAALIMU

Ndalichako apingwa na walimu Maswa. Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani hapa, Mkoa wa Simiyu, kimemjia juu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako kuwa anaupotosha umma juu ya madai yao. Kimesema walimu wanadai madeni mengi, hivyo kauli ya Ndalichako kwamba hawana wanachodai inalenga kuleta uchonganishi kati yao na Serikali. Mwenyekiti wa CWT wilayani hapa, Onesmo Makota amesema wao wanaidai Serikali zaidi ya Sh500 milioni kutokana na malimbikizo na mapunjo ya mishahara.

Magazeti ya leo september 28

Magazeti ya Leo September 28.9.2016 Magazeti ya Leo September 28.9.2016...

Serikali kuzindua leo ndege mpya

September 27, 2016 VIDEO: Ndege mpya ya pili ya Air Tanzania ilivyowasili jijini Dar es salaam Newsroom TZA Baada ya ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuwasili nchini September 20 2016, Leo September 27 2016  ndege yapili ya Bombadier Q400 imewasili Dar es salaam ikitokea Canada baada ya ile ya kwanza ambazo zimenunuliwa na serikali. Naambiwa kuwa uzinduzi rasmi wa ndege hizo utafanyika kesho jumatano September 28 2016 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere Dar es salaam. ULIKOSA HII NDEGE MPYA YA KWANZA ILIVYOWASILI JIJINI DAR ES SALAAM? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

LUKUVI AFUTA HATI TATU MAKABURI KINYERENZI

Serikali yafuta hati 3 eneo la makaburi kinyerezi Wakazi wa Kinyerezi Sokoni, Dar es Salaam wameipongeza Serikali ya awamu ya Tano kwa kufuta hati tatu zilizokuwazimetolewa katika eneo la makaburi liliouzwa kinyume cha sheria. Pongezi hizo zimetolewa leo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi baada ya kumwagiza kamishna wa ardhi Kanda ya Dar es Salaam kufuta hati hizo mara moja na kulirejesha eneo la makaburi kwa wananchi. Akiongea kwa niaba ya wakazi wa Kinyerezi, Mwanasheria, Mwinjuma Mzee amesema kuwa Wanakinyerezi wanamshukuru sana Mhe. Waziri kwa kurejesha eneo la makaburi kwa wakazi hao. “Mhe. Waziri na msafara wake wote tunawashukuru kwa kumaliza mgogogoro huu ambao umedumu kwa muda mrefu na tumemwomba Waziri ashughulikie na maeneo mengine yanayohusu huduma za jamii kama zahanati na shule,” alisema Mzee. Naye mkazi wa Kinyerezi, Bi. Maimuna Forogo ameelezea furaha yake kwa kumshukuru sana Mhe waziri kwa hatua aliyoichukua ya kuba...

MATUMAINI WIZARA YA DAWA

Wizara yasema dawa zinapatikana kwa asilimia 53 Dar es Salaam. Serikali kupitia Wizara ya Afya imewaondoa wasiwasi watanzania kuhusu uhaba  wa dawa nchini na kueleza kuwa dawa zinapatikana kwa asilimia 53. Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk Mpoki Ulisubisya amesema hali ya upatikanaji wa dawa itaimarika zaidi mwanzoni mwa Oktoba. Amesema kati ya dawa muhimu 135 zinazohitajika,ghalani zipo aina 71 na nyingine zipo kwenye vituo vya kutolea huduma.

UGONJWA WAZINAA-KISONONO

Dalili za ugonjwa wa zinaa - kisonono Kisonono ni ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa, ugonjwa huu hutokana na wadudu aina ya Neisseria gonorrhoeae. Ugonjwa huu pia huambukizwa kwa tendo la ngono na hata kutoka kwa mama mjamzito anapojifungua huweza kumuambukiza pia mtoto endapo atakuwa alikuwa nao. Ugonjwa wa kisonono kwa mara nyingi huwapata vijana na watu wazima. Waathirika wengi wa ugonjwa huu wa kisonono huambatana na magonjwa mengine ya zinaa, kwasababu kunabaadhi ya magonjwa mengine ya zinaa hujificha bila kuonyesha dalili, hivyo kukuta ukiugulia ndani kwa ndani. Ugonjwa wa kisonono, unazuilika na kutibika pia, unaposikia dalili zozote za magonjwa ya zinaa, unashauriwa kumchukua mwenzi wakona kuwahi hospitali  kuchukua vipimo kwaajili ya matibabu. DALILI ZA UGONJWA WA KISONONO. Mara nyingi ugonjwa wa kisosnono huwa hauonyeshi dalili yoyote mwanzoni. Lakini ukionyesha dalili basi kwa mwanaume utasikia maumivu makali wakati wa kukojoa na kuambatana na usaha kutoka uumeni...

MAGONJWA HATARI 10

Magonjwa hatari 10 yanayotibika kwa kutumia mbegu za maboga Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki, kopa, maginizia, manganizi na chuma, mbegu za maboga ni tamu na zinaweza kutafunwa nyakati zozote na mahali popote hasa kwa wapenda kutafuna-tafuna kama mimi. Tafiti mbalimbali zimethibitisha pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida nyingi kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10 yafuatayo: 1. UGONJWA WA MOYO Kiasi kingi cha madini ya magnesium katika mbegu za maboga yanazifanya mbegu hizi kuwa mhimu sana kwa watu wenye magonjwa mbalimabli ya moyo. Madini ya magnesium ni mhimu kwa ajili ya kuimarisha msukumo wa damu kwenye moyo na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hatimaye kutibu na kuzuia magonjwa ya moyo. Mbegu hizi pia zina mafuta mengine mhimu zaidi kwa watu wenye ugonjwa wa moyo yenye OMEGA 3. 2. HUIMARISHA KINGA YA MWILI Mbegu za maboga zimebarikiwa kuwa na kiasi cha kutosha cha madini...

Serikali ya kishetani

Shetani yuko duniani, na anafanya kazi duniani. Watu wengi wanapokua wanapambana na shetani wanakua wanawaza kwamba yuko mbali sana na wao. Shetani amewakilishwa na majina mbali mbali katika biblia; mfano > Shetani > Ibilisi > Mwovu Shahidi nane kibiblia zinazoonyesha shetani anakaa duniani. 1. Shetani alitupwa duniani Ufunuo 12:12 2. Shimo la kuzimu lipo hapa hapa duniani Ufunuo 9:1-2,11 3. Siku moja alionekana duniani anazunguka zunguka. Ayubu 1:7, ayubu 2:2 Shetani anazunguka zunguka na pia anatembea tembea. Hivyo unaweza kukutana nae anatembea, au anazunguka zunguka. Bwana aliongea na shetani ili sisi tuweze kujifunza kutoka Kwenye maongezi yake. 4. Shetani aligombania mwili kwenye mazishi. Kumbu 34:1-6 Hapa biblia inaonyesha Musa amekufa,na Mungu akamzika. Lakini Yuda 1:9 shetani akashindana na mikaeli kwa ajili ya mwili wa Musa. 5. Shetani aliingia kwenye ibada wakati Kuhani mkuu Yoshua akiendesha ibada Zekaria 3:1-2 6. Shetani aliongea na Daudi. 1 Nyakati 21:1 7. Duni...

WALIOMKAIDI MAGUFULI WAANZA KUSHUHULIKIWA

SAKATA la wafanyabiashara watano waliogoma kulipa kodi ndani ya muda uliowekwa na Rais John Magufuli limechukua sura mpya baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwakabidhi kwenye vyombo vya dola kwa hatua za kisheria. Wafanyabiashara hao ni miongoni mwa 43 ambao awali walitajwa kupitisha makontena 329 bandarini bila kuyalipia kodi. Mwishoni mwa mwaka jana, Rais Magufuli alitoa siku saba wajisalimishe wenyewe kulipa kodi kwa TRA bila adhabu. Akizungumza na Nipashe ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA, Richard Kayombo alisema kutokana na muda uliotolewa kuisha na wafanyabiashara hao kushindwa kutekeleza walichoagizwa vyombo vya dola vinaendelea kulifanyia kazi suala hilo ili hatua za kisheria zichukuliwe. Alisema wameamua kuvishirikisha vyombo vya dola kwa sababu wafanyabiashara hao wamekiuka agizo lililotolewa awali la kuwataka walipe kodi kwa hiyari yao ndani ya muda waliopewa. Alisema makampuni ya wafanyabiashara hao...

CUF YATOA TAMKO ZANZIBAR

Kaimu Mkurugenzi wa habari, uenezi na mawasiliano kwa umma Ismail Jussa. Kufuatia taarifa iliyotolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho iliyokutana Zanzibar juzi, tarehe 27 Desemba, 2015, waandishi wengi wa habari wametupigia simu wakitaka kujua Chama Cha Wananchi (CUF) kimepokea vipi taarifa ile. Vikao vya CCM ni vikao vya CCM. Si kawaida yetu kutolea taarifa maamuzi ya vikao vya vyama vyengine. Hata hivyo, tunaelewa ni kwa nini kumekuwepo na shauku ya kusikia CUF inasema nini kwa sababu yale yaliyokuwemo kwenye taarifa hiyo yaligusia pia mazungumzo yanayofanyika Ikulu Zanzibar yanayolenga kupata ufumbuzi wa mgogoro wa uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015. Baada ya kuipitia taarifa ya CCM na mengine yaliyoelezwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar wakati akitoa ufafanuzi wa yale yaliyomo kwenye taarifa hiyo, CUF tunapenda kuwaeleza Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla haya yafuatayo: 1. Taari...